Alaaa! Atwoli adai Afisa Mkuu wa Safaricom Peter Ndegwa ni hatari

Katibu Mkuu wa Muungano wa vyama vya wafanyikazi Francis Atwoli amemshtumu Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya Safaricom Peter Ndegwa kwa kile alichokitaja kama kutojali maslahi ya wafanyikazi.

Kwenye taarifa, Atwoli amesema Ndegwa anatilia maanani sana kuongeza pato la kampuni hiyo bila kujali wafanyakazi waliokuza kampuni hiyo hadi kufikia kiwango cha wateja milioni 30.

Also Read
Wanafunzi 36,254 waliofanya KCPE 2020 kujiunga na shule za upili za kitaifa

Atwoli ameitaka Bodi ya Wasimamizi ya Kampuni hiyo ya mawasiliano kumfuta kazi Ndegwa iwapo hataghairi mtindo wake wa uongozi ambao unalenga kupunguza wafanyikazi kupitia mabadiliko ya usimamizi.

“Japo Ndegwa ndiye Afisa Mkuu Mtendaji wa kwanza Mkenya, ndiye afisa hatari zaidi ambaye kampuni hiyo imewahi kupata hasa ukizingatia ulinzi wa haki za wafanyikazi,” akasema Atwoli.

Also Read
Martha Koome: Sibanduki katika kamati ya kuandaa uchaguzi

Katibu huyo wa COTU amedai kwamba hatua ya Ndegwa ya kuwataka baadhi ya waajiriwa wa Safaricom kutuma upya maombi ya kazi katika nafasi wanazoshikilia kwa sasa imezua wasiwasi miongoni mwa wafanyakazi.

Amesema hatua hiyo inalenga kupunguza idadi ya wafanyikazi hao ambao kwa sasa ni zaidi ya 6,000 na pia ni kinyume na azimio la shirika la kimataifa kuhusu wafanyakazi ILO.

Also Read
Wakili John Khaminwa adai maisha yake yamo hatarini

Huku akikariri kwamba COTU haina udhibiti wa moja kwa moja wa mtindo wa usimamizi, Atwoli amesema muungano huo una wasi wasi kuhusu maslahi ya wafanyikazi hao.

COTU sasa imemtaka Peter Ndegwa kusitisha mpango huo kwa sasa ambao Atwoli anasema unasababisha msongo wa mawazo miongoni mwa wafanyakazi.

  

Latest posts

Dereva na Makondakta wawili watiwa nguvuni kwa kukiuka sheria za trafiki

Tom Mathinji

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi