Australia kuwatumia wanajeshi kutekeleza masharti dhidi ya Covid-19

Australia imewapeleka mamia ya wanajeshi jijini Sydney kutekeleza vikwazo vya kuzuia kusambaa kwa Covid-19.

Takriban visa elfu-3 vya maambukizi na vifo tisa vimetokana na chamko la aina mpya ya virusi vya Delta lililochipuza mwezi Juni.

Wanajeshi wa Australia watapata mafunzo mwishoni mwa juma hili kabla ya kuanza doria bila silaha siku ya Jumatatu.

Also Read
Museveni awakashifu polisi wanaowatesa raia

Kuanzia siku ya Jumatatu, wanajeshi 300 watawasaidia polisi kuenda nyumba hadi nyumba kuhakikisha waliothibitishwa kuwa na Covid-19 wanajitenga, hayo ni kwa mujibu wa afisa mkuu wa polisi wa South Wales Mick Fuller.

Also Read
Kenya yatemwa nje ya FIBA Afrobasket kufuatia kipigo cha pointi 58-60 na Sudan Kusini

Hatua hiyo ya kufungwa kwa shughuli itakayoendelea hadi tarehe 28 mwezi ujao, inawazuia watu kuondoka kwenye makazi yao isipokuwa kwa mazoezi muhimu, kununua bidhaa, utunzaji na sababu nyingine.

Licha ya kufungwa kwa shughuli kwa majuma matano, visa vya maambukizi katika jiji hilo kubwa zaidi nchini humo vimeendelea kuongezeka.

Also Read
Kenya yajiunga na nchi zingine kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika

Maafisa siku ya Ijumaa, wamenakili visa 170 vipya. Wanajeshi wataungana na polisi kwenye maeneo yenye idadi kubwa ya visa vya maambukizi ya virusi hivyo ili kuhakikisha wakazi wanatii kanuni zinazojumuisha kusafiri kwa eneo la kilomita 10 pekee.

  

Latest posts

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

NCIC kuwatumia vijana kuwa mabalozi wa amani kabla ya msimu wa uchaguzi

Tom Mathinji

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuvuruga amani hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi