Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Serikali imewaagiza wakurugenzi wa elimu katika kaunti kuwatambua wanakandarasi watakaojenga madarasa ili kuhakikisha mfumo wa elimu wa CBC unatekelezwa kwa urahisi.

Wizara ya elimu imetoa muda wa hadi mwezi Aprili mwaka ujao kukamilishwa kwa awamu ya kwanza ya mradi huo, ambao utasababisha kujengwa kwa madarasa 11,600 kwa matayarisho ya kusajiliwa kwa wanafunzi wa mfumo huo katika shule za upili mwaka wa 2023.

Also Read
Visa vipya 1,091 vya maambukizi ya korona vyanakiliwa humu nchini

Waziri wa elimu profesa George Magoha amewaagiza wakurugenzi hao kuhakikisha wananchi wa kawaida wanashirikishwa kwenye miradi hiyo.

Also Read
Ruto aonya dhidi ya kutumia taasisi za serikali kisiasa

Kundi linalojumuisha washirika mbali mbali, likiongozwa na wizara ya elimu pamoja na wizara ya usalama walikutana siku ya jumatano kupanga mikakati ya hawamu ya pili ya utekelezaji wa mfumo wa elimu wa CBC.

Waziri wa usalama Dkt. Fred Matiang’i ametoa onyo kwa machifu watakaokosa kuhakikisha madarasa yamejengwa katika maeneo yao.

Also Read
Kamati ya bunge kuhusu Afya yataka taasisi ya KEMRI kuongezewa ufadhili

Shule zote za upili nchini zitakuwa na kitengo cha shule ya upili ya daraja la chini maarufu junior secondary, huku usajili wa kwanza kwa wanafunzi hao ukitarajiwa mwaka 2023.

  

Latest posts

John Nkengasong: Omicron sio virusi vipya vya Covid-19

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi milioni 2 za chanjo aina ya AstraZeneca kutoka Ujerumani

Tom Mathinji

Watu 96 zaidi waambukizwa COVID-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi