Azawi Ashauri Wanamuziki Wenza

Mwimbaji na mwandishi wa nyimbo nchini Uganda Azawi amehimiza wanamuziki wenzake wajizatiti na kuandaa kazi za ubora wa hali ya juu. Kulingana naye, hiyo ndiyo njia pekee wataweza kushindana na wanamuziki wa kimataifa.

Azawi alipata kujulikana baada ya kusajaliwa na kampuni ya kurekodi muziki na usimamizi wa wanamuziki ya Swangz Avenue. Ujuzi wake katika kuandika nyimbo na kuimba umesababisha kazi zake zipate kupendwa barani kote.

Also Read
Siku nitakufa mnizike mara moja! Akothee

“Wasanii tunalalamika kwamba serikali haitusaidii lakini tunafaa kukumbuka tunashindana na ulimwengu ili tutilie maanani kinachoendelea katika ulingo wa muziki ulimwenguni.” alisema binti huyo.

Mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Priscilla Zawedde anasema wanamuziki wa Uganda wanaweza kuafikia umaarufu kama wa wanamuziki wa Afrika Magharibi ikiwa watanoa kazi zao.

Also Read
Josky Kiambukuta ameaga dunia!

Anahisi kwamba wanamuziki wa Nigeria wanaelewa biashara ya muziki na hushindana na ulimwengu na wala sio wenyewe kwa wenyewe.

Azawi aliingilia sanaa ya muziki baada ya kuzuru kituo cha utamaduni cha Ndere na alianza na kucheza densi katika kundi la Kika mwaka 2005. Baadaye aliachana na kundi hilo na kuangazia uimbaji na uandishi wa nyimbo.

Also Read
Winnie Nwagi Asema ni Wakati wa Azawi Kung'aa

Wanamuziki ambao ameandikia nyimbo ni pamoja na Lydia Jazmine, Nina Roz na Eddy Kenzo.

  

Latest posts

Regina Daniels Ajifungua Mtoto wa Pili Kwenye Siku ya Kuzaliwa ya Kifungua Mimba Wake

Marion Bosire

Msanii Aandaa Maonyesho ya Kuhamasisha Kuhusu Historia ya Rwanda

Marion Bosire

Lamar Odom Yuko Tayari Kurudiana na Taraji P. Henson

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi