Azimio waafikiana kuwasilisha kesi katika mahakama ya upeo kupinga matokeo ya kura za Urais

Viongozi waliochaguliwa wa muunagno wa  Azimio la Umoja One Kenya wameidhinisha hatua ya kuwasilisha kesi katika mahakama ya upeo kupinga kutangazwa kwa William Ruto kuwa Rais mteule na  tume ya IEBC.

Kiongozi wa muungano huo Raila Odinga siku ya Jumatano katika jumba la mikutano ya KICC alisema tayari wamefahamishwa kuhusu hatua ya kuwasilisha kesi na wamekubali kwa kauli moja.

Also Read
Kenya imejiandaa vilivyo kukabiliana na aina mpya ya Covid-19

“Leo tumekuwa na kikao cha kufahamiakiana na viongozi waliochaguliwa kwa muungano wetu kutoka kote nchini na kuweka mikakati ya kwenda mbele .

“Tumewaelezea kuhusu uchaguzi wa Urais  na wameidhinisha”akasema Raila

Kikao hicho kimewaleta Pamoja viongozi waliochaguliwa kwa tiketi ya muungano wa Azimio wakiwemo magavana,maseneta,waakilishi wa akina mama na wabunge.

Also Read
Mahakama yaondoa maagizo ya kuzuia IEBC kusitisha usajili wa wapiga kura

Mwanaiji mwenza wa Raila,Martha Karua amesema kuwa ushindi wa muungano huo umecheleweshwa tu lakini bado watapata ushindi na haki kupitia kwa mahakama  ya upeo.

“Ushindi wetu umeahirishwa  tu lakini tutaupata ,huu ndio ujumbe wetu kwa Wakenya” akasema Karua

Also Read
Shujaa kuchuana na Australia kuwania nafasi ya kwanza kundi D michezo ya jumuiya ya madola

Kiongozi wa chama cha Wiper leader Kalonzo Musyoka alisema bado wataendelea kupambana huku akiwa na Imani ya ushindi.

“Hatua yetu ya kupinda matokeo ya kura za Urais imevutia ulimwengu mzima na tuko tayari kuhakikisha taifa haliendi katika upande mbaya “akasema  Musyoka

  

Latest posts

NPS: Oparesheni ya kiusalama Turkana yazaa matunda

Tom Mathinji

Bodi ya dawa na sumu yapiga marufuku uuzaji wa dawa ya kupanga uzazi ya ‘Sophia’

Tom Mathinji

Bunge la kitaifa na la Seneti kuanza vikao vyao Jumanne

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi