Baada ya miaka mine mafichoni, Albert Lelei akamatwa kwa mauaji ya Inspekta wa Polisi

Hatimaye Albert Lelei Ntuitai, ambaye ni mshukiwa wa mauaji ya aliyekuwa Inspekta Mkuu wa Polisi Henry Odongo Sindani miaka mine iliyopita, ametiwa mbaroni.

Mshukiwa huyo amekuwa mafichoni tangu mwaka wa 2016 baada ya kutekeleza mauaji ya inspekta huyo.

Also Read
Kenya yanakili visa 925 vipya vya Covid-19 huku watu 15 zaidi wakifariki

Kabla ya kuuawa kwake, Odongo alikuwa Afisa Mkuu wa Polisi katika Kituo cha Polisi cha Kigumo, Kaunti ya Murang’a.

Kulingana na taarifa ya Idara ya Upelelezi wa Uhalifu (DCI), Lelei, amaye alikuwa dereva wa polisi, alifika kazini mnamo tarehe 26 mwezi Juni mwaka wa 2016, baadaye akaanza kugombana na mkubwa wake kisha akampiga risasi tisa na kutoweka.

Tangu siku hiyo, mshukiwa huyo amekuwa akikwepa majaribio kadhaa ya kunaswa.

Also Read
COVID-19: Afisi za Kaunti ya Kirinyaga zafungwa kwa muda
Also Read
Gavana wa Nairobi Mike Sonko abanduliwa mamlakani

Hata hivyo, alikamatwa na maafisa wa upelelezi siku ya Jumamaosi kwenye eneo la Senetoi, Kaunti Ndogo ya Narok Kusini na anatarajiwa  kujibu mashtaka yanayomkumba.

  

Latest posts

Mutahi Kagwe: Wahudumu wa afya wafeli katika somo la Kingereza

Tom Mathinji

Prof Magoha: Awamu ya kwanza ya ujenzi wa madarasa ya CBC kukamilika mwezi Aprili mwakani

Tom Mathinji

Benki ya dunia kuipa Kenya shilingi bilioni 16.7 kukabilia na ukame

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi