Baba aliyembaka bintiye wa miaka 6 Kisii kufikishwa mahakamani

Mwanamume anayedaiwa kumnajisi bintiye mwenye umri wa miaka sita wiki iliyopita katika Kaunti ya Kisii anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Maafisa wa Idara ya Upelelezi walimkamata Julius Ogamba Ongera ambaye alitoweka baada ya kutekeleza uovu huo katika kijiji cha Megogo, Marani, Kaunti ya Kisii.

Also Read
Mwanafunzi akamatwa akiwa na kisu darasani Kwale

Mshukiwa huyo alitiwa nguvuni jana na maafisa wa DCI wakisaidiwa na wenzao wa huko Kisii, mahala alikokuwa amejificha huko Kongasis, Kiambogo, katika Kaunti ya Nakuru.

Inasemekana Ongera alimshawishi binti wake kwenda kichakani ambako alitekelezea unyama huo.

Makachero hao walisema Ongera alimtishia mke wake endapo angefichua habari hizo kwa polisi.

Also Read
Washukiwa wawili wakamatwa kwa kuwawekea watu dawa katika vinywaji kabla kuwaibia

Msichana huyo alipatikana kwenye shamba la kahawa na wanakijiji akiwa na uchungu mwingi na kupelekwa haraka kwenye Hospitali ya Kaunti Ndogo ya Marani kabla ya kuhamishwa hadi Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Kisii kwa matibabu maalum.

Also Read
Uvuvi haramu katika ziwa Naivasha wakabiliwa

Habari za kisa hicho ziliwakera Wakenya wengi zilipopakiwa kwenye mitandao ya kijamii, hasa picha zilizoonyesha jinsi nguo za msichana huyo zilivyolowa damu.

Ongera atafikishwa mahakamani leo kujibu mshtaka kuhusu kisa hicho.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi