Baba aliyezoea kumnajisi bintiye mwenye umri wa miaka 13 hadi kumpachika mimba akamatwa

Mwanamume mwenye umri wa miaka 35 amekamatwa kwa madai ya kumnajisi bintiye mara kadhaa na hatimaye kumpachika mimba.

Ephram Kimani Macharia alitiwa nguvuni siku ya Jumamosi na maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Uhalifu (DCI) katika eneo la Kigumo, Kaunti ya Murang’a.

Also Read
DCI yawakamata washukiwa wanaolaghai watu kwa kigezo cha kuwatafutia wapenzi

Kulingana na taarifa ya DCI, msichana huyo mwenye umri wa miaka 13 ni mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi ya Gatumbi.

Taarifa hiyo inasema kwamba mwalimu mkuu wa shule hiyo aligundua hali ya msichana huyo isiyokuwa ya kawaida na akaamua kumpeleka hospitalini ambako alifanyiwa uchunguzi na kugundulika kuwa mja mzito wa miezi sita.

Also Read
Wafugaji watakiwa kutumia mbinu za kisasa za ufugaji

Baada ya kuhojiwa, msichana huyo alifichua kwamba babake mzazi ndiye mhusika wa uja uzito, huku akikiri kwamba babake amekuwa akimnajisi tangu mwezi Julai mwaka wa 2020.

Also Read
Wakazi wa Dodoma kutazama mwili wa Magufuli Jumapili

Msichana huyo sasa amewekwa chini ya uangalizi wa afisa wa kushughulikia maswala ya watoto kwenye kituo kimoja cha uokoaji katika eneo la Muthithi, naye mshukiwa akiwekwa kizuizini huku uchunguzi ukiendelea.

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi