Babake Winnie Nwagi kumsimamia kama meneja

Mkataba wa mwanamuziki wa Uganda Winnie Nwagi wa miaka miwili na kampuni ya kusimamia wanamuziki ya Swangz Avenue utatamatika mwaka huu.

Kampuni hiyo iko tayari kuongeza mkataba wa kusimamia mwanamuziki huyo lakini babake kwa jina Henry Kabiito anataka kuchukua usukani kama meneja wa Binti yake.

Mzazi huyo amesikika mara nyingi akisema kwamba binti yake hafaidi kifedha kutokana na mkataba aliotia saini na kampuni hiyo ya Swangz.

Also Read
Mahakama ya ICC yamfunga miaka 25 gerezani, aliyekuwa kiongozi wa waasi wa Uganda Dominic Ongwen

Mzee Kabiito ana imani kwamba binti yake atapata pesa nyingi kutoka kwa muziki wake akiwa chini ya usimamizi wake.

Kabiito anasema ana fedha za kutosha kufadhili mahitaji ya mwanawe kimuziki.

Also Read
Marekani yataka kuchunguzwa kwa ghasia za uchaguzi nchini Uganda

Winnie Nakanwagi maarufu kama Winnie Nwagi wa umri wa miaka 30 sasa aliingia kwenye ulingo wa muziki nchini Uganda kupitia kwa awamu ya pili ya shundano la “Coca-cola Rated Next” mwaka 2014 ambapo alimaliza katika nafasi ya tatu.

Baadaye alisajiliwa na kampuni ya Swangz Avenue ambapo amerekodi vibao kadhaa na kilichofanya vyema zaidi ni “Musawo” cha mwaka 2016.

Also Read
E - Sir akumbukwa

Aliwahi kuolewa na mwanamuziki mwenza Valentino Rukundoye Joshua maarufu kama C’zabu na wakajaliwa mtoto mmoja lakini ndoa yao haikudumu.

Winnie Nwagi anafahamika pia kwa kibao “Kwata Essimu” ambacho amemshirikisha msanii Freeboy.

  

Latest posts

Waigizaji Wa Nollywood Wazuru Zanzibar kwa Fungate

Marion Bosire

Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Marion Bosire

Gurdian Angel Asifia Mpenzi Wake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi