Babu wa Loliondo aliyepata umaarufu wa kutibu magonjwa sugu amefariki

Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu kwa jina la ‘Babu wa Loliondo’, ambaye alipata umaarufu wa kutoa tiba ya kikombe kilichokuwa kinadaiwa kutibu magonjwa mbalimbali amefariki dunia.

Kulingana na gazeti la Mwananchi la nchini Tanzania, taarifa za kufariki kwa mchungaji Mwasapile, zilithibitishwa na mmoja wa waliokuwa wasaidizi wa mzee huyo, Paul Dudui zilizosema kuwa mzee Mwasapile alifariki Ijumaa Julai 30, 2021 mchana katika kituo Cha Afya Cha Digodigo baada ya kuugua ghafla.

Also Read
Wapiganaji wa kigeni watakiwa kuondoka nchini Libya

“Nikweli mzee amefariki muda huu ndio tunasubiri mwili uletwe hapa chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya Wasso” alisema Dudui

Also Read
Kipsang' asajili rekodi mpya ya Olimpiki na kuingia fainali ya mita 1500 sawia na Cheruiyot wakati Simotwo akifungiwa nje

Kwa mujibu wa gazeti hilo la Mwananchi, Dudui alisema mwili huo ulitarajiwa kupokea na viongozi wa Serikali wa Wilaya na kabla ya kutoa taarifa rasmi.

Mnamo mwaka 2011, Mchungaji Mwasapile mwenye umri wa miaka 86, aligonga vichwa vya habari baada ya maelfu watu kufurika nyumbani kwake kupata tiba asili iliyosemekana kutibu magonjwa mengi.

Also Read
Marekani yarejea katika mkataba wa Paris kuhusu hali ya hewa

Hata hivyo, iliripotiwa na vyombo vya habari nchini humo kuwa watu 52 waliaga dunia wakisubiri kupokea tiba ya Mchungaji huyo.

  

Latest posts

Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Watumishi wa Umma wahimizwa kushirikisha taasisi mbali mbali kufanikisha majukumu yao

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi