Bahati Apoteza Yote

Siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, mwanamuziki Bahati alitoa madai kadhaa baada ya kushauriwa atupilie mbali azma yake ya kuwania ubunge eneo la Mathare. Muungano wa Azimio la umoja One Kenya ulibuni mpango wa kuhakikisha unanyakua viti vingi vya ungune katika kaunti ya Nairobi. Mpango huo ulihusu kugawia vyama vya muungano huo maeneo bunge ya kuwa na wawaniaji huku wa vyama vingine vilivyo chini ya muungano huo wakishauriwa kujiondoa.

Also Read
Sossio ashtumiwa kwa kutotetea vilivyo chama cha KNUT

Eneo bunge la Mathare liliachiwa chama cha ODM na kwa sababu hiyo Bahati ambaye alikuwa anawani kupitia chama cha Jubilee akashauriwa ajiondoe lakini akakataa. Alifanya kikao na wanahabari wakati huo akitiririkwa na machozi akielezea jinsi ameambiwa ajiondoe na akasihi viongozi wa muungano huo wampe fursa ya kutafuta uongozi. Katika harakati hizo alidai kwamba aliahidiwa kazi serikalini pamoja na pesa nyingi ili ajiondoe lakini akakataa.

Also Read
Wiki ya Shukrani

Kabla ya majibu ya uchaguzi kutangazwa katika eneo bunge la Mathare, Bahati kupitia Instagram alidai kwamba masanduku 21 ya kura yalikuwa yameharibiwa na kwamba hakukuwa na shughuli yoyote katika kituo hicho siku tatu baada ya siku ya kupiga kura.

Kulingana na matokeo ya mwisho kutoka eneo bunge hilo, Anthony Oluoch wa chama cha ODM amehifadhi kiti chake kwa kura 28,098 akafuatiwa na mwaniaji wa chama cha UDA Billian Ojiwa kwa kura 16,912. Bahati alishika nambari tatu kwa kura 8,166. Sasa mwimbaji huyo amekosa kiti hicho cha ubunge na pesa na kazi serikalini vitu ambavyo alisema aliahidiwa na muungano wa Azimio la Umoja One Kenya.

  

Latest posts

Wakazi wa Baragoi wahimizwa kuishi kwa amani

Tom Mathinji

NHIF yaongeza muda wa kuwapa bima ya afya maafisa wa Polisi

Tom Mathinji

Moses Kuria avunja chama chake na kujiunga na UDA

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi