Bahati azuru Afrika Kusini

Mwanamuziki Kevin Mbuvi Kioko, maarufu kama Bahati yuko jijini Johannesburg nchini Afrika Kusini kwa ajili ya ziara na kutumbuiza kama mwanamuziki.

Yeye ni mmoja wa wanamuziki ambao watatumbuiza kwenye tamasha kwa jina “Africa Day Concert” litakaloandaliwa huko Afrika Kusini.

Tamasha hilo litaendeshwa na Idris Elba ambaye ni mwanamuziki na muigizaji maarufu kutoka uingereza ila ana asili ya Afrika. Babake Idris ni mzaliwa wa Sierra Leone na mamake ni mzaliwa wa Ghana ambao walioana nchini Sierra Leone kabla ya kuhamia London Uingereza.

Also Read
Amber Lulu aota kaolewa na Diamond!

Tamasha hilo la Afrika limedhaminiwa na MTV Base Africa na mtandao wa YouTube ambapo litapeperushwa kwenye runinga ya MTV na kwenye mtandao wa You Tube tarehe 25 mwezi huu wa Mei mwaka 2021.

Bahati anasema yeye ndiye msanii pekee kutoka Kenya ambaye atatumbuiza siku hiyo. Mwaka jana, kundi la Sauti Sol liliwakilisha Kenya kwenye tamasha sawia.

Also Read
DNG Azungumzia Mkutano wa Wasanii na Naibu Rais

Wasanii watakuwa kwenye majukwaa kadhaa siku hiyo ambayo yatakuwa kwenye nchi kama vile Kenya na Nigeria na hilo linatokana na janga linaloendelea la virusi vya Corona ambalo linafanya iwe vigumu kwa watu kukusanyika.

Orodha kamili ya watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo haijulikani lakini akiwa Afrika Kusini, Bahati amekutana na mwanamuziki wa Tanzania Diamond Platnumz ambaye anaendelea kuandaa albamu yake.

Bahati alimshukuru Diamond kwa ushauri ambao anasema ni muhimu wakati huu ambapo yeye mwenyewe anaandaa albamu yake.

Malkia wa WCB Zuchu naye amepachika picha ambazo zinamwonyesha akiwasili Afrika Kusini isijulikane kama yuko pale kwa ajili ya tamasha la Afrika au albamu ya Diamond.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi