Baada ya kutikisa na kusababisha minong’ono kwenye mitandao ya kijamii, mwanamuziki Kevin Bahati na mke wake Diana wamejitokeza kusema kwamba bado wako pamoja na kwamba ilikuwa ni kioja tu cha kujitafutia wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.
Mambo yalianza pale ambapo Diana alitoa picha zote za mume wake kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii akidai kwamba ameachana naye.
Wawili hao kuanzia hapo walianza kuandika maneno kwenye mitandao kuashiria kwamba bado wanapona kutokana na kuachana kwao.
Inatokea kwamba wawili hao wameshirikiana kwa mara ya kwanza kwenye wimbo ambao unaitwa “Mtaachana tu” na ilikuwa njia ya kuvutia watu ndio wawape wimbo. Wameomba msamaha kwa kuhadaa wafuasi wao na wakasema wataelezea sababu ya kufanya hivyo baadaye.
Diana naye amejawa na furaha kwani ni mara yake ya kwanza kuimba au kushirikishwa kwenye wimbo.
Wimbo huo unazinduliwa saa sita hii leo kwenye mitandao ya kijamii.