Bahati Kuwania Ubunge wa Mathare

Msanii wa muziki nchini Kenya Kelvin Kioko maarufu kama Bahati ametangaza kwamba atawania kiti cha ubunge cha eneo la Mathare katika kaunti ya Nairobi kwenye uchaguzi mkuu wa tarehe tisa mwezi Agosti mwaka 2022. Mwimbaji huyo ambaye anamiliki kampuni ya muziki ya EMB atawania wadhifa huo kupitia chama cha Jubilee.

Bahati alilelewa katika eneo bunge la Mathare katika kituo cha watoto yatima kiitwacho ABC baada ya wazazi wake kuaga dunia akiwa mdogo. Alipata elimu ya msingi na sekondari chini ya makao hayo ambapo alikamilisha mwaka 2011. Mwaka 2012, Bahati aliingilia kazi ya muziki akianza kama mwimbaji wa nyimbo za injili za kisasa na baadaye mwimbaji wa nyimbo za kidunia.

Also Read
Bahati na Diana : Kibao Kipya
Also Read
KFCB Yapiga Marufuku Filamu Inayoshabikia Ushoga

Bahati ana mke mmoja kwa jina Diana Marua mzaliwa wa kaunti ya Migori na pamoja wana watoto wawili Heaven na Majesty. Bahati ana mtoto mkubwa msichana kwa jina Mueni na mpenzi wake wa zamani Yvette.

Kando na Bahati wapo wanamuziki wengine ambao wamejitosa kwenye ulingo wa siasa kama vile Roy Smith Mwatia maarufu kama Rufftone ambaye anawania useneta wa kaunti ya Nairobi kupitia chama cha UDA. Mwingine ni Bi. Loice Kim ambaye anawania kiti cha mwakilishi wa kike wa kaunti ya Kiambu bungeni kupitia chama sawa na Rufftone.

Also Read
Bahati Azungumza Kuhusu Kufurushwa Kutoka Mkutano wa Azimio la Umoja

Mchekeshaji Jasper Muthomi maarufu kama MC Jessy naye anawania ubunge wa Imenti Kusini kupitia chama cha UDA.

  

Latest posts

Harusi ya Nandy Kuwa ya Awamu Tatu

Marion Bosire

Mwigizaji Mkongwe wa Nollywood Kenneth Aguba Apata Usaidizi

Marion Bosire

Travis Baker Arejea Kazini

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi