Bahati Kuzindua Albamu yake

Kevin Mbuvi Kioko maarufu kama Bahati mwanamuziki hapa nchini Kenya alianza kwa kujitambulisha kama mwanamuziki wa nyimbo za injili ambazo aliimba kwa muda hadi mwaka jana ambapo aligura na kuanza kuimba za kidunia.

Baadaye alitoa nyimbo kadhaa za mapenzi akiwa ameshirikisha wasanii kama vile Mejja kwenye kibao Dear X, Tanasha Donna katika kibao One and Only na Vivian kwenye wimbo Najua.

Wiki kama saba zilizopita Bahati aliaandaa kambi na wote wanaohusika na kazi yake ya muziki kwa ajili ya kutayarisha albamu yake na sasa iko tayari.

Also Read
"Atakaye kunioa ajue mimi ni madhabahu" Rose Muhando

Albamu hiyo kwa jina “Love Like This” itazinduliwa Jumapili tarehe 13 mwezi Juni mwaka 2021 katika hoteli ya TradeMark. Jumatatu tarehe 14 mwezi Juni mwaka huu wa 2021 albamu hiyo itapatikana kwenye jukwaa la mitandaoni la BoomPlay.

Wageni waalikwa pamoja na wanahabari watahitajika kuvaa mavazi ya rangi nyeusi, nyekundu na rangi ya dhahabu.

Haya yanajiri baada ya mwanamuziki Bahati kutoa wimbo kwa jina “Fikra za Bahati”. Kwenye wimbo huo anakashifu wanamuziki kadhaa akielezea pia sababu ya kugura sekta ya nyimbo za injili.

Ametaja wasanii kama vile Ringtone ambaye anamtania kwa kupendelea umbea kwa hivyo anamvisha kanga na Octopizzo ambaye anadai aliendewa kwa mganga kwani alipata mzungu akashindwa kujipanga.

Wengine ambao amewazungumzia ni Khaligraph Jones au ukipenda Omollo ambaye anapenda sana kufanya mazoezi wa kujenga misuli na Daddy Owen ambaye alinyanganywa mke.

Rafiki yake Bahati ambaye pia ni mwanamuziki na ambaye amesalia kwenye muziki wa injili DK Kwenye Beat alijibu wimbo huo akimkosoa Bahati kwa maneno ambayo alitupia wengine. Kwenye video ya wimbo wake mfupi wa jibu, DK amebeba msalaba ambao huwekwa kwenye kaburi ambao una maelezo kuhusu Bahati.

Maneno hayo kwenye msalaba yanasema kwamba alizaliwa kwenye muziki wa injili na amefia kwenye muziki wa kidunia.

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi