Na Judith Akolo.
Mkurugenzi wa kituo cha kuthibiti magonjwa barani Afrika anayeondoka Dkt. John Nkengasong, ametaka mataifa yanachama ya muungano wa Afrika kutumia fursa ya kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19, kuimarisha utafiti wa chanjo dhidi ya ugonjwa huo.
Akizungumza kwenye hotuba yake ya kila wiki, Dkt. Nkengasong alisema hatua hiyo itasaidia mataifa ya Afrika kukabiliana na uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa huo.
Dkt. Nkengasong pia alielezea masikitiko yake kwamba jitihada za kuhakikisha kuna chanjo ya kutosha barani humu zinatatizwa na idadi ndogo ya watu wanaojitolea kupata chanjo hiyo.
Wiki hii, Afrika imeripoti visa vipya 50,000 vya maambukizi ya ugonjwa huo, huku mataifa matano yakirekodi idadi ya juu zaidi ya maambukizi yakijumuisha Afrika Kusini, Zimbabwe, Tunisia, Eswatini Namibia.
Uchumi za mataifa ya bara Afrika ulisambaratishwa na virusi hivyo, kwa kuwa biashara nyingi zikifungwa, huku viwanda vya uzalishaji bidhaa vikifungwa.