Bara la Afrika lasifiwa kwa kudhibiti Covid-19

Kituo cha udhibiti wa magonjwa Barani Afrika kimeyasifia mataifa ya bara hili kwa kupunguza kusambaa kwa virusi vya Covid-19.

Mkurugenzi wa kituo hicho John Nken-Gasong amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na maafisa wa afya Barani humu zilisaidia kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.

Also Read
Wanajeshi wa Eritrea wajiondoa kutoka eneo la makabiliano la Tigray nchini Ethiopia

Nken-Gasong alitaja madai kwamba idadi kamili ya vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo barani humu haviripotiwi ipasavyo kuwa si ya kweli.

Kufikia sasa bara la Afrika limenakili zaidi ya visa milioni 1.4 vya ugonjwa wa Covid-19 ambapo watu 34,000 wameripotiwa kuaga dunia tangu mwezi Machi mwaka huu.

Idadi hiyo ni ndogo kuliko ile iliyoripotiwa Katika mataifa ya bara Ulaya, Asia na Marekani huku maambukizi mapya yakiendelea kupungua.

Also Read
Kundi la waasi lauteka mji wa Bangassou katika Jamhuri ya Afrika ya Kati huku mapigano yakiendelea
Also Read
Wakuu wa Jeshi wajiuzulu nchini Brazil

Bara Afrika lililo na watu zaidi ya bilioni moja limenakili chini ya asilimia tano ya maambukizi ya ugonjwa huo na asilimia 3.6 ya vifo vilivyotokana na virusi hivyo hatari.

  

Latest posts

Mgomo wa wahudumu wa afya wasababisha maafa Guinea Bissau

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika azikwa Jijini Algiers

Tom Mathinji

Aliyekuwa Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika amefariki

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi