Barabara ya kwanza ya mwendo kasi ya kulipia Afrika Mashariki yaanza kufanya kazi kwa majaribio

Na Kelly Ogome & Tom Wanjala.

Barabara ya mwendo kasi ya Nairobi inayounganisha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta na mji wa Nairobi imeanza kufanya kazi kwa majaribio.

Barabara hiyo iliyojengwa na kampuni ya China ni ya kwanza ya mwendo kasi ya kulipia katika ukanda wa Afrika Mashariki, na inafuatiliwa sana na wenyeji wa huko katika siku za karibuni.

Watu wamesema, “Barabara hii itasaidia kupunguza msongamano wa magari kati ya nyumbani na ofisini, na itatusaidia kufika mahali kwa wakati. Inakadiriwa kuwa nauli ya mabasi itapungua vilevile. Kuna njia nyingi kwenye kila upande wa barabara hiyo, hivyo tunatumai barabara hiyo inaweza kuturahisishia safari zaidi. Nafuatilia ujenzi wa barabara hii kila siku.”

Baada ya barabara ya Thika kufanyiwa ukarabati mwaka wa 2012, uchumi wa nchi ulianza kupanuka, na hata pato la taifa kuongezeka kwa asilimia tano kila mwaka. Kwa sasa baada ya kujengwa kwa Express Way, ninatarajia kwamba uchumi utaimarika zaidi.

Viongozi wakubwa wanaokuja kwenye mikutano ya kimataifa hapa Nairobi watakuwa wanatumia muda mfupi sana kutoka uwanja wa ndege hadi jijini Nairobi. Vile vile, bidhaa kama vile maua zitasafirishwa kwa haraka sana hadi uwanja wa ndege ili kusafirishwa nchi za nje. Kutokana na jinsi ilivyojengwa, hii barabara itavutia wawekezaji wengi sana.”

“Tangu Nairobi Express ijengwe na Wachina, imependeza sana. Imefanya jiji la Nairobi linavutia mno. Hata mimi hutumai siku moja nitapiga picha nikiwa kwenye Express Way ili niweke kwenye mitandao ya kijamii. Yaani Nairobi kwa sasa inapendeza! Halafu pia mazingira mazuri huwapa watu nguvu ya kufanya kazi. Hii barabara inawafurahisha sana wakazi wa Nairobi ambao bila shaka watachapa kazi yao vizuri.”

Also Read
Peter Kenneth: Mlima Kenya uko huru kuwa na mgombeaji Urais

Barabara hiyo si kama tu ni mradi wa miundombinu, bali pia ni mradi unaohusiana na maisha ya watu, na kuongeza nafasi za ajira. Mkurugenzi wa kituo cha kushughulikia mambo ya ETC ya barabara hiyo George Karimi amesema, nafasi elfu tatu za ajira zilitolewa kwenye kipindi cha ujenzi wa barabara, na kuzinufaisha kampuni 200 za ujenzi na mamia ya makampuni ya vifaa vya ujenzi ya huko.

Pia, nafasi 500 za ajira zitatolewa kwenye kipindi cha uendeshaji, ikiwa ni pamoja na nafasi za kazi ya ETC.

Bw. George Karimi amesema, “Naweza kukwambia kuwa wafanyakazi wenyeji walioko kituoni ni kati ya 300 hadi 450. Katika kituo hiki tuko na mfanyakazi mmoja wa China.

Mafunzo tuliyopata ni ya huu mfumo mpya kwa sababu hii ndio mara ya kwanza kutumia ETC Kenya.

Kwa hivyo tumejifunza kuhusu kifaa hiki cha ETC. ”Barabara ya mwendo kasi ya Nairobi ina urefu wa kilomita 27.1 yenye kasi ya kilomita 80 kwa saa, na inaunganisha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, kitovu cha eneo la biashara jijini Nairobi, Ikulu ya Kenya na sehemu nyingine.

Baada ya barabara hiyo kuanza kutumika, muda wa usafiri wa kipindi cha kilele utapungua hadi dakika 15 hadi 20 kutoka masaa mawili ya awali kwenye barabara ya Mombasa, hali ambayo itapunguza sana msongamano wa magari pamoja na gharama ya usafiri wa magari, na kuongeza ufanisi wa usafiri mjini.

Also Read
Koome: Rais Kenyatta anapaswa kuwateua majaji sita waliotemwa nje

Samwel Ndungu ni mhandisi hodari wa sekta ya ujenzi nchini Kenya, ambaye ameshiriki ujenzi wa Nairobi Express Way.

Ameeleza sababu ya kuchagua kampuni ya China kujenga barabara hiyo.Bw. Samwel Ndungu amesema, “Kenya imefaidika sana kutoka kwa ujuzi wa China katika ujenzi wa mtandao wa barabara za mwendo wa kasi. Kampuni za Kichina zina miundombinu imara ambazo wahandisi wa Kenya hawana uzoefu kutumia. Kwa hivyo, serikali ya Kenya imepiga hatua kubwa sana katika uimarishaji wa miundombinu na miradi mingine ya kusaidia raia wake kama vile barabara ya Nairobi Express Way. Kando na mradi huu wa Express Way, barabara zingine kuu, barabara za kipekee za kutumiwa na mabasi, barabara za mashinani na miradi mingine imetekelezwa na kampuni za ujenzi za Kichina.”

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya alipokagua barabara hiyo mwaka 2019 alisema, ujenzi wa barabara ya Nairobi ni kazi ngumu kutokana na hali ya utatanishi ya njia.

Ikiwa ni mradi wa kwanza wa ushirikiano kati ya serikali ya Kenya na sekta binafasi na umma, Nairobi Express inajengwa na Kampuni ya Uhandisi wa Madaraja na Barabara ya China ikishirikiana na serikali ya Kenya chini ya mpango wa ujenzi, uendeshaji na uhamishaji (BOT). Kwenye mradi huo, China inawajibika na uwekezaji, ufadhili, uhandisi, ujenzi, uendeshaji na ukarabati.

Also Read
Google kutoa msaada wa shilingi bilioni 10 kwa kenya kupiga jeki ufufuzi wa uchumi

Hivi karibuni, mashindano ya kwanza ya Marathon ya jiji la Nairobi yalifanyika kwenye barabara hiyo. Kwenye hafla ya kutoa tuzo, Rais Uhuru alisema kutokana na miundombinu ya kisasa kama Nairobi Expressway, sekta za utalii, biashara na uwekezaji nazo zitanufaika.

Rais Uhuru Kenyatta, amesema, “Express Way mpya ambayo tumejenga katika mji wetu wa Nairobi itatusaidia kumaliza msongamano wa magari ambao unakumba mji huu wetu wa Nairobi huku tukizidi kuimarisha jiji letu. Katika mfumo wa majaribio, tutafungua hii barabara ili wananchi waweze kuitumia kwa magari. Kwa hivyo Wakenya wenzangu, barabara itakuwa wazi kutumiwa na magari na wananchi.”

Richard Mutisya amebahatika kuwa dereva wa kwanza kuendesha gari lake kwenye barabara hiyo tangu ilipofunguliwa rasmi.

Bw. Richard Mutisya amesema, “Unajihisi vizuri unapoendesha gari kwenye barabara hiyo. Kuna changamoto nyingi unapotumia barabara ya chini. Kando na msongamano wa magari, moshi unaotolewa na haya magari unachafua hewa na kuhatarisha maisha ya watu. Express Way imesaidia mambo mengi sana. Nairobi itafaidika sana.”

Ikiwa ni mradi muhimu wa ushirikiano wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, mradi wa Nairobi Express ulianzishwa rasmi tarehe 16 mwezi Oktoba mwaka 2019, na thamani yake ya ujenzi ni karibu dola milioni 600 za kimarekani.

Ikiwa ni barabara ya kulipia, muda wa uendeshaji wa mradi huo ni miaka 30, ikiwa ni pamoja na miaka mitatu ya ujenzi na mingine 27 ya uendeshaji. Baada ya muda kumalizika wa miaka 30, Kenya itapewa bure mali na vifaa vyote.

  

Latest posts

Mataifa ya G7 kusitisha uagizaji dhahabu kutoka Urusi

Tom Mathinji

Mzozo wa Ukraine na Russia kujadiliwa katika mkutano wa G7

Tom Mathinji

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia augua Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi