Baraza awarai wakaazi wa Bungoma kujiandikisha kwa wingi kupiga kura

Mwaniaji wa kiti cha ugavana kaunti ya Bungoma Zacharia Baraza Siuma ,  amewarai wakaazi kujitokeza kwa wingi kujisajili kuwa wapiga kura , ili kufanya maamuzi ya busara katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti mwaka huu.

Kwa mjibu wa Baraza tume huru ya mipaka na uchaguzi IEBC,  inapaswa kufanya uhamasisho wa umma ,kabla ya kuanza kuwaandikisha wapiga kura Jumatatu ijayo ya Januari 17 .

Baraza akihutubia wananchi kaunti ya Bungoma

“IEBC haindikishi watu wengi kwa sababu ya kukosa kufanya uhamasisho ,akitaka watu wapige kura unatakiwa kufunza kabla ya kuanza kuwaandikisha “akasema Baraza

“Mimi mwanzo nawaomba watu wa Bungoma kujitokeza kwa wingi kupiga kura ,na sio tu kujiandikisha ,hakikisha ukienda kupiga kura chagua  mtu aliye na maono ya kubdialisha kaunti,wenyewe waangalie mtu walio na maono,mimi ningeomba watu wapigie UDA ili waone UDA kama itabadilisha kaunti ya Bungoma ,baada ya Ford Kenya kushindwa licha ya kutoa viongozi kaunti za Bungoma na Tranz Nzoia “akaongeza  Baraza

Also Read
Naibu Gavana wa Makueni Adelina Mwau ajiunga na chama cha UDA

“Mambo nitakayoyapa kipa umbele,ni kuhakikisha kuwa tunafufua viwanda ili watu wawe na pato na waondoke kwenye ufukara,pia katika afya tutaweka facilities ambazo zitatoa huduma kwa wakaazi badala ya kuenda nje ya kaunti kutafuta matibabu,kutoa mbegu kwa wakulima na kuhakikisha watoto wote wanapata elimu “akasisitiza  Baraza

Also Read
Watu kadhaa wahofiwa kufariki kwenye ajali ya moto Busia

Mfanyibiashara huyo pia amempongeza  kiongozi wa mashtaka ya umma Noordine Hajji , kwa kuanza kuwachukulia hatua viongozi wanaowachochea Wakenya  na kuitaka pia tume ya kitaifa ya  maridhiano na utangamano wa kitaifa NCIC kumsaidia DPP kuwaadhibu wahusika wa uchochezi.

“Ningependa kumpongeza na pia kumshukuru  DPP kwa hatua aliyochukua ya kuwaadhibu viongozi wachochezi haswa huu ukiwa mwaka wa uchaguzi itakuwa vizuri kwa ofisi ya DPP na pia tume ya NCIC kuzima  uchochezi,   ili tusiwe na machafuko ya baada ya uchaguzi”akasema Baraza

Haya yajiri siku chache baada ya  seneta wa Meru Mithika Linturi na mbunge wa Kitutu Chache Richard Onyonka kuwashtakiwa kwa  kutoa matamshi ya uchochezi wiki iliyopita.

Also Read
IEBC kutumia sajili za vitabu na zile za ki elektroniki Jumanne

Zacharia ambaye atawania Ugavana wa Bungoma kwa tiketi cha United Democratic Alliance(UDA),amesema atalenga kubadilisha hali ya uchumi wa kaunti hiyo  ikiingia afisini.

Tume ya IEBC  inalenga kuwasili wapiga kura milioni 4 nukta 5 kote nchini , katika awamu ya pili ya usajili wapiga kura baina ya Januari 17 na Februari 6 mwaka huu.

Kuhusu uchaguzi wa Urais ,mwanabiashara huyo anaamini kuwa kinyang’anyiro kitakuwa baina ya Raila Odinga na  William Ruto .

 

  

Latest posts

Kamati ya Kusaidia Rais Mteule Kuchukua Hatamu za Uongozi Yaanza Kazi Rasmi

Marion Bosire

Didmus Barasa Ajisalimisha kwa Maafisa wa Polisi

Marion Bosire

Gavana Mandago Sasa ni Seneta

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi