BASATA Yaagizwa Kugharamia Matibabu ya Mwanamuziki Tanzania

Waziri wa utamaduni, Sanaa na michezo nchini Tanzania Mheshimiwa Innocent Bashungwa ameagiza Baraza la Sanaa la Tanzania – BASATA kwa ushirikiano na Chama cha Muziki na Dansi Tanzania – CHAMUDATA limpeleke hospitalini mwanamuziki wa muda mrefu nchini humo Mzee Hussein Abdallah Stima.

Also Read
Gigy Money amefilisika?

Mzee huyo wa umri wa miaka 85 anaugua ugonjwa wa moyo na shinikizo la damu tangu mwaka jana.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo leo baada ya kumzuru Mzee Hussein nyumbani kwake katika eneo la Buguruni kwa Mnyama huko Dar es Salaam.

Also Read
Wasafi Tv yarejea hewani

Mzee Hussein Abdallah Stima alishukuru waziri na serikali kwa msaada huo huku akitoa ushauri kwa wanamuziki wa sasa kuimba nyimbo za kuhamasisha umma kuhusu maendeleo na uzalendo.

Also Read
Sound from Segerea - Dullvani amtania Rayvanny

Mzee huyo anafahamika sana kwa uwezo wake wa kupuliza ala ya Saxophone kwenye bendi kadhaa kama vile Cuban Marimba.

  

Latest posts

Brown Mauzo Azindua Video ya Kibao “Naoa”

Marion Bosire

Wadau wa Filamu Wahimizwa Kutoa Mawasilisho ya Warsha ya Durban

Marion Bosire

Akothee Atangaza Ziara

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi