Basket Mouth asema anataka kuzunguka sanaa zote

Bright Okpocha mchekeshaji wa Nigeria ambaye wengi wanamfahamu kama Basket Mouth amesema kwamba nia yake ni kuzunguka kwenye sekta zote za sanaa na sio tu kuonja bali kuibuka mshindi.

Akizungumza kwenye mahojiano na Legit.ng jukwaa la habari za Nigeria kwenye mitandao ya kijamii, Basket Mouth alisema alianzia uchekeshaji, akasonga akaingia kwenye kuigiza vipindi vya runinga kisha akaigiza kwenye filamu za Nollywood na amefanya muziki. Mwishowe anataka kurejea kwenye uchekeshaji ambapo alianzia.

Also Read
Nkechi Blessing aomba msamaha hadharani

Bright anasemekana kuwa tayari amejaza albamu ya muziki na amehusisha wasanii tajika kwenye vibao kadhaa vya albamu hiyo na jina lake la muziki ni Basket. Albamu hiyo aliizindua mwezi Disemba mwaka 2020.

Alifunguka pia kuhusu mipango aliyokuwa nayo awali kuhusu kufungua klabu cha uchekeshaji na anasema mipango hiyo ilitimia na klabu hicho kimekuwepo kwa muda wa miezi miwili sasa.

Also Read
Sound Sultan afariki

Huwa anaigiza kwenye kipindi chake ambacho kinaitwa “Papa Benjy” ambacho alianzisha mwisho wa mwaka jana na mazingira yake ni eneo la kuuzia chakula maarufu nchini Nigeria, “Pepper Soup”.

Kulingana naye, kipindi chake kinahitaji muziki kidogo katikati na ndio maana aliamua kuimba nyimbo zake ili asije akajipata pabaya kisheria kwa kutumia miziki ya wengine kutokana na haki miliki.

Also Read
Njoro anaomboleza

Wasichojua wengi ni kwamba kipawa ambacho Bright Okpocha alitangulia kugundua maishani ni kucheza ngoma na baadaye muziki aina ya rap katika kundi la “Da Psychophats”.

kitu kingine ni kwamba ana kamuni ya kusimamia wanamuziki na kuwarekodia nyimbo kwa jina “Barons World Entertainment” ambayo alianzisha mwaka 2014.

  

Latest posts

Betty Bayo Afichua Sura ya Mpenzi Wake

Marion Bosire

Mr. Seed Asimulia Safari Yake ya Muziki

Marion Bosire

Rick Ross Azungumzia Uhusiano Wake na Hamisa Mobeto

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi