BBI: Mabunge saba yapitisha mswada wa marekebisho ya katiba

Mchakato wa marekebisho ya katiba kupitia mpango wa maridhiano ya kitaifa (BBI) unazidi kupamba moto huku jumla ya mabunge saba ya kaunti yakiwa tayari yamepitisha mswada huo.

Bunge la Kaunti ya Kajiado katika eneo la Bonde la Ufa limekuwa la hivi punde kupitisha mswada huo wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020.

Kaunti hiyo imefuata mkondo wa zile za Siaya, Kisumu, Homa Bay, Pokot Magharibi , Trans Nzoia na Busia.

Hadi sasa ni Bunge la Kaunti ya Baringo pekee ambalo limekatalia mbali mswada huo.

Mabunge mengine kadha yakiwemo Nairobi, Embu, Kakamega, Laikipia na Kiambu yameandaa vikao vya kupokea maoni ya umma kuhusiana na mswada huo, huku Nairobi na Laikipia yakitarajiwa kuujadili Alhamisi.

Baadhi ya kaunti ziliwaalika wataalam kuhamasisha umma kuhusu mswada huo na pia kujibu maswali yao kuhusiana na ripoti hiyo ya BBI.

Mswada huo uliungwa mkono kwa kauli moja kwenye kaunti tano ingawaje kulikiwa na wachache waliodai kwamba mswada huo utakuwa mzigo kwa wananchi.

  

Latest posts

Mama Taifa ampongeza Jim Nyamu kwa juhudi zake za kuwatunza Ndovu

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 1,335 zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Nyumba za thamani ya shilingi milioni 10 zabomolewa Kitui

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi