Bebe Cool asema alilipwa pesa nyingi

Mwanamuziki wa Uganda Moses Ssali maarufu kama Bebe Cool ameendelea kutetea hatua yake ya kuhusika katika safari ya wanamuziki kwenye eneo la kaskazini mwa nchi hiyo la Gulu mradi ambao uliendelea kwa muda wa mwezi mmoja.

Akizungumza kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga huko Uganda, Bebe Cool alisema kuna pesa katika biashara ya muziki lakini lazima mtu awe na njia mwafaka za kufikia na kuchukua fursa zilizopo.

Also Read
Ushindani kati ya Bebe Cool na Bobi Wine

Wakati huu wa janga la Corona ambalo limeathiri mno sekta ya burudani kwa jumla, Bebe Cool anasema alilipwa milioni 400 pesa za Uganda kwa kufika kwenye eneo fulani, kutagusana na wanamuziki wengine na kutumbuiza kidogo, kwa hivyo sio pesa zilimpeleka Gulu maanake tayari alikuwa nazo.

“Kabla ya janga la Corona, nilipata kazi na mpango wa Guinness night football na nililipwa milioni 400. Pesa zingeongezeka hata zaidi lakini matukio yalokuwa yamepangwa katika eneo la Afrika Mashariki yalitupiliwa mbali kwa sababu ya janga hili.” alielezea Bebe Cool.

Also Read
Daniel Kaluuya - Mganda aliyeng'aa kwenye tuzo za Oscar

Baadhi ya wanamuziki kama vile Bobi Wine, hawakuridhishwa na hatua ya wenzao ya kuongoza wanaochipuka kwenye fani ya muziki kwenda kuhudhuria mikutano ya General Salim Saleh huko Gulu ambapo wanasemekana kuvutiwa na pesa. Hata hivyo Bebe Cool amekanusha hilo akisema walikwenda pale kujifunza kuhusu jinsi ya kujipatia pesa katika biashara ya muziki.

Also Read
Joeboy awasili Tanzania

Bebe Cool anaamini kwamba mradi ulioendeshwa na General Saleh na wanamuziki umekuza utamaduni mpya katika sekta ya burudani nchini Uganda.

Wanamuziki, watayarishaji muziki, wapiga muziki yaani Deejays, wachekeshaji, mameneja wa wasanii kati ya wengine wengi kwenye sekta ya burudani wamekuwa wakiishi Gulu kwa zaidi ya mwezi mmoja ambapo wanaaminika kupata mafunzo.

  

Latest posts

Aki Na Paw Paw Warejea

Marion Bosire

Harmonize Atoa Orodha Ya Nyimbo Za Albamu Mpya

Marion Bosire

Watayarishaji Filamu Waalikwa Kutoa Kazi Zao Kwa Tamasha La Filamu La Durban Mwaka Ujao

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi