Bei ya Mafuta Kusalia Ilivyo kwa Mwezi Mmoja Ujao

Mamlaka ya kudhibiti bei ya mafuta na ile ya kawi EPRA imetangaza kwamba bei ya mafuta itasalia ilivyo kwa muda wa mwezi mmoja ujao. Mamlaka hiyo huwa inabadilisha bei ya mafuta tarehe 14 kila mwezi na leo imetoa taarifa ya kuashiria kwamba bei ambayo imekuwepo itaendelea kutumika.

Also Read
Watu milioni 27 kuchanjwa dhidi ya Covid-19 kufikia mwezi Juni mwaka 2022

Bei ya mafuta aina ya super petrol itasalia kuwa shilingi 159.12, dizeli shilingi 140.00 na mafuta taa shilingi 127.94 kwa kila lita katika eneo la Nairobi.

Also Read
Rais Kenyatta azindua mfumo wa kitaifa wa habari kuhusu ardhi

Kwenye taarifa hiyo EPRA ilifafanua kwamba serikali itaendelea kutumia ruzuku ili kuondolea wakenya mzigo wa bei ya juu ya mafuta. Chini ya mpango huo wa ruzuku lita moja ya mafuta aina ya super petrol imelipiwa na serikali shilingi 54.91, dizeli shilingi 66.17 na mafuta taa yamelipiwa shilingi 74.17.

Also Read
Watu watatu wafariki katika ajali ya barabarani lari

Huko Mombasa bei ya mafuta aina ya super petrol, mafuta taa na dizeli ni shilingi 156.56, 137.76 na 125.69 mtawalia.

  

Latest posts

Malkia Strikers warejea nyumbani kinyemela baada ya kubanduliwa mashindano ya dunia

Dismas Otuke

CAF yafungua maombi ya maandalizi ya fainali za AFCON mwaka 2025

Dismas Otuke

NHIF yaongeza muda wa kuwapa bima ya afya maafisa wa Polisi

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi