Ben Pol aanzisha taratibu za kisheria kumtaliki Anerlisa Muigai

Ripoti kutoka Tanzania zinaashiria kwamba mwanamuziki Ben Pol ameandikisha talaka hiyo katika mahakama ya Mwanzo jijini Dar Es Salaam.

Ben Pol au ukipenda Benard Michael Paul Mnyang’anga hajatangaza hayo hadharani lakini duru za kuaminika zinathibitisha kwamba ni kweli.

Anerlisa Muigai ambaye anamiliki kampuni kwa jina Nero ambayo inapakia na kuuza maji alifunga ndoa na mwanamuziki huyo nchini Tanzania mwisho wa mwezi mei mwaka 2020, muda mfupi baada ya mazishi ya dadake Anerlisa kwa jina Tecra.

Also Read
Anerlisa Muigai athibitisha talaka

arusi yao ilifanyika katika kanisa katoliki la Mtakatifu Gaspar eneo la Mbezi Beach, jijini Dar es salaam.

Ben Pol alihudhuria mazishi ya Tecra ambapo alionekana kukubalika kwenye familia hiyo ya wafanyibiashara ambayo inamiliki kiwanda cha kutengeneza pombe cha Keroche.

Tangu wakati huo,ndoa ya wawili hao imekuwa ya panda shuka pale ambapo Anerlisa alikuwa anafika muda anafuta picha zake na mume wake na baadaye wanaonekana pamoja.

Also Read
Ragga Dee apuuza Bobi Wine

Zamu hii amefuta na hawajaonekana tena pamoja na huenda ndio mwisho.

Anerlisa yuko Kenya ambapo anaendeleza biashara yake na Ben Pol yuko nchini Tanzania ambapo anaendelea na kazi ya muziki na ile ya kutetea mazingira kwani yeye ni balozi wa hazina ya mazingira ya ulimwengu yaani WWF nchini Tanzania.

Also Read
Olu Jacobs, muigizaji mkongwe nchini Nigeria

Ben Pol hajafuta picha za pamoja na Anerlisa ingawaje sio nyingi na muda mwingi huwa nchini Tanzania. Millard Ayo, mwanahabari wa Tanzania aliripoti kuhusu mwanzo wa taratibu za talaka mahakamani kati ya Ben Pol na Anerlisa akisema haieleweki ni kwa nini mwanamuziki huyo amechukua hatua kama hiyo.

  

Latest posts

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Eduswagga Azungumzia Safari Yake Ya Muziki

Marion Bosire

Tory Lanez Afuta Instagram Kulikoni?

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi