Benjamin Ayimba ahitaji msaada wa shilingi milioni 2 nukta 2 za matibabu

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya raga ya Kenya kwa wachezaji 7 kila upande Benjamin Ayimba anahitaji shilingi milioni 2 nukta 2 ili kupokea matibabu maalum katika hospitali ya Kenyatta.
Ayimba ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya taifa kwa sasa amelazwa katika kitengo cha wagonjwa wa kujitegemea katika Hospitali ya Nairobi ambapo anaugua malaria ya ubongo wakihitaji zaidi ya shilingi milioni mbili ili apokeaa matibabu katika hospitali ya Kenyatta.
Ayimba anakumbukwa kuwa kocha bora wa timu ya taifa alipoingoza kushinda taji kuu katika mashindano ya Singapore 7’s mwaka 2016.
Wahisani wanaweza kutuma mchango wa pesa kupitia Paybill 8021673 ,jina la akaunti Benjamin Ayimba.
  

Latest posts

Shujaa yaangukia kundi moja na Uhispania,USA na Chile mkondo wa Edmonton 7’s

Dismas Otuke

Tegla Lorupe balozi wa amani kupitia michezo

Dismas Otuke

Kenya Lionesses kuvaana na Msumbiji kuwania tiketi ya robo fainali FIBA Afrobasket

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi