Benjamin Netanyahu ang’atuliwa mamlakani

Utawala wa miaka 12 wa waziri mkuu wa Israeli Benjamin  Netanyahu, umefika Kikomo baada ya bunge la nchi hiyo kuunga mkono kubuniwa kwa serikali ya muungano.

Serikali hiyo mpya ya mabadiliko iliyopigiwa kura Jumapili, itaongozwa na Naftali Bennett wa chama cha Yamina anayeegemea mrengo wa kulia.

Also Read
Tanzania kupokea dozi 500,000 aina ya Pfizer kufikia mwisho wa mwezi Oktoba

Bennett aliyeapishwa kuwa Waziri mkuu wa Israeli, ataongoza serikali hiyo ya muungano wa vyama vingi iliyoidhinishwa kwa kura hafifu 60 dhidi ya kura 59.

Bennett atahudumu wadhifa wa waziri mkuu hadi mwaka 2023 kulingana na mkataba wa ugavi wa mamlaka.

Also Read
Watu 714 zaidi waambukizwa Covid-19 hapa nchini

Kisha atakabidhi mamlaka kwa Yair Lapid ambaye ni kiongozi wa chama cha Yeah Atid kwa kipindi cha miaka miwili.

Netanyahu ambaye anakabiliwa na madai ya ufisadi kwenye kesi inayoendelea, amebadilisha siasa za Israeli kwa miaka mingi.

Also Read
Rais wa Brazil awakosoa magavana waliofunga shughuli za uchumi kudhibiti Covid-19

Jumamosi  usiku, takriban waandamanaji elfu mbili walikusanyika nje ya makazi ya kiongozi huyo aliye na umri wa miaka 71, kusherehekea kile walichoamini kuwa kuondoka kwake mamlakani.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Tanzania kupokea dozi 500,000 aina ya Pfizer kufikia mwisho wa mwezi Oktoba

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi