Betty Kyallo Apata Kazi ya Kuigiza

Aliyekuwa mtangazaji wa runinga Betty Kyallo ametangaza kwamba amepata kazi ya kuigiza na pia kuwa afisa wa kutangaza filamu moja ya kimataifa. Kyallo ambaye alipata umaarufu kutokana na kuwa mtangazaji wa taarifa kwa lugha ya kiingereza kwenye runinga, alitumia mitandao ya kijamii kutangaza habari hizo njema.

Alipachika picha akiwa na jamaa kwa jina Jamal Kibet Collins na anaonekana akitia saini mkataba wa kazi hiyo ambayo inaitwa “The Great Gamble”.

Also Read
Tuzo za Kalasha

Kulingana na Betty mswada wa filamu hiyo ijayo uliibuka wa tatu kwenye shindano la waandishi wa miswada ya filamu kati ya miswada 2,447 iliyokuwa imewasilishwa toka kote ulimwenguni.

Mama huyo wa mtoto mmoja ambaye sikuhizi anafanya biashara anasema ana furaha kushirikiana na wakenya wenzake katika kuunda filamu hiyo ambayo itasambazwa na “Miramax Films”.

Also Read
Idris Elba atangaza ujio wa kibao chake na Megan Thee Stallion

Katika tangazo lake, Betty Kyallo amemtaja muigizaji Sarah Hassan, Studio za Big Tools na Miramax Films. Hii ndio mara ya kwanza Betty atakuwa anaigiza kwenye filamu baada ya kuwa mmoja wa waliohusishwa kwenye video ya wimbo “My Jaber” ambao ni ushirikiano kati ya kundi la Har_t the Band na Brizy Annechild.

Also Read
"Uhalifu na Haki"

Willis Raburu ambaye ni mwanamuziki na mtangazaji amempongeza Betty kwa kazi hiyo ambayo amepata sawia na Terryanne Chebet ambaye amemwandikia, “Wow!!!! Congratulations always Betty!”.

  

Latest posts

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Kipindi Cha Wendy Williams Kuendelezwa na Watangazaji Tofauti

Marion Bosire

“Upendo” Kibao Kipya Kutoka Kwa Zuchu Na Spice Diana

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi