Beyonce asema mwaka 2020 umembadilisha

“Nafurahikia kabisa muda wa kukaa na familia yangu, lengo langu sasa ni kupunguza mwendo na kuondoa mambo ya kunifadhaisha maishani.”

Ndiyo maneno aliyoyasema mwanamuziki nyota wa muda mrefu wa Marekani Beyonce wakati wa mahojiano na Edward Enninful, ambaye ni mhariri mkuu wa jarida la British Vogue.

Picha ya Beyonce ndiyo iko kwenye jalidi la jarida hilo toleo la mwezi Disemba mwaka 2020.

Mwanamuziki huyo alielezea kwamba amekuwa kwenye fani ya muziki tangu akiwa na umri wa miaka 15 na tangu wakati huo amekuwa tu akifanya kazi ya kurekodi na kuzindua muziki bila kupumzika.

Also Read
Rayvanny kuzindua albamu

Kulingana naye ni vigumu mtu kupitia janga kama hili la Corona na kuona watu wakiandamana kupigania haki katika sehemu mbali mbali ulimwenguni na akose kubadilika.

“Nilizindua albamu ya ‘Lemonade’ wakati wa ziara ya ulimwengu, nikajifungua watoto mapacha, nikatumbuiza kwenye ‘Coachella’, nikaelekeza ‘Homecoming’, nikakwenda ziara nyingine ya ulimwengu na mume wangu, alafu kukaja ‘Black Is King’ na yote hayo yalifuatana.

Also Read
Khaligraph amshinda eric Omondi

Kazi imekuwa nzito na ya kuchosha nimekuwa nikiangazia tu urithi wangu na kuwakilisha utamaduni wangu ipasavyo ila sasa nataka niangazie yanayonipa furaha.” Aliendelea kusema.

Beyonce aliolewa na mwanamuziki mwenzake Jay Z mwaka 2008 na pamoja wamebarikiwa na watoto watatu ambao ni Blue Ivy msichana aliyezaliwa mwanzo wa mwaka 2012 na mapacha Rumi wa kike na Sir wa kiume ambao wanakaribia kutimiza miaka mitatu tangu kuzaliwa.

Also Read
Mshauri wa Trump kuhusu Covid-19 Scott Atlas, ajiuzulu

Mwimbaji huyo wa miaka 39 sasa alifichua kwamba alipojifungua mwanawe wa kwanza aligundua uwezo ambao ako nao na uzazi umekuwa msukumo katika kazi zake tangu wakati huo.

Aliamua kujitolea kuhakikisha kwamba mwanawe anaishi katika dunia ambayo anahisi yuko salama na anathaminiwa.

Baada ya kubarikiwa na mtoto mvulana anasema ameelewa pia umuhimu wa kuinua mtoto wa kiume na kuhakikisha anapata kila anachohitaji, anafahamu historia na anajithamini mwenyewe.

 

  

Latest posts

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Eduswagga Azungumzia Safari Yake Ya Muziki

Marion Bosire

Tory Lanez Afuta Instagram Kulikoni?

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi