Beyonce asherehekea watoto wake

Mwanamuziki tajika nchini Marekani Beyoncé amesherehekea siku ya kuzaliwa ya watoto wake wawili mapacha kwa maneno matamu. Rumi na Sir wametimiza umri wa miaka minne na Beyonce hawezi kuficha furaha yake kama mzazi.

Kwenye tovuti yake ya kibinafsi Beyonce aliandika, “Ni kipi bora zaidi ya zawadi moja … ni mbili” na kumalizia kutakia watoto hao siku njema ya kuzaliwa.

Mshindi huyo wa tuzo 28 za Grammy na mume wake Jay Z walijaliwa watoto hao mapacha mwaka 2017 na wana kifungua mimba wao wa umri wa miaka 9 binti kwa jina Blue Ivy.

Also Read
Mwanamuziki Bow Wow kuingilia mieleka

Katika umri huo wake mdogo, Blue Ivy tayari ni mshindi wa tuzo la Grammy. Tuzo hilo lilitokana na video ya wimbo ambao alishirikishwa na mamake Beyonce, na wanamuziki Saint JHN na WizKid.

Kupitia kwenye mahojiano miaka ya awali, wanandoa Jay Z na Beyonce na watu wao wa karibu wamefichua jinsi wanatekeleza kazi ya malezi ya watoto wao watatu.

Also Read
Kamala Harris aongoza watu wengine mashuhuri kumkumbuka George Floyd

Hata ingawa wawili hao huwa na kazi nyingi ambazo wakati mwingine huwa zinahitaji kusafiri mbali kwa muda mrefu huwa wanajitahidi kupata muda na wanao.

Mwezi Aprili mwaka huu, Jay Z alihojiwa na jarida la Sunday Times ambapo alielezea kwamba kuwapa watoto mapenzi ya dhati ni jambo la muhimu pamoja na kuwapa nafasi ya kuchagua njia ya kufuata maishani.

Alisema hawezi kulazimisha wanawe kurithi biashara zake.

Also Read
Ujauzito wa Amber Rutty waharibika

Mamake Beyonce kwa jina Tina Knowles ambaye ni mwanamitindo alifichua kwamba Beyonce haamini katika kuchapa watoto kama njia ya kuwaadhibu ila huwa anajadiliana nao na hiyo ndiyo njia alimlea Beyonce.

Kufatia uamuzi wao wa kuacha watoto wachague watakachokuwa maishani, inaonekana kwamba Blue Ivy amechagua njia ya muziki kama wazazi wake. Yeye huandamana na mamake kila mara anapokwenda nje kwa kazi za muziki na huwa anashirikishwa kwa baadhi ya vibao vyake.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi