Biashara ya bidhaa za Afrika kwa njia ya mtandao wa Internet kupanua mauzo ya bidhaa za Afrika nchini China

Na Fadhili Mpunji.

Mwezi Aprili mwaka huu shughuli nyingi ya mauzo bidhaa za Afrika kwenye mtandao wa internet ilifanyika nchini China.

Wateja wa miji mbalimbali ya China walitumia muda wao kwenye simu na kompyuta zao, wakitazama, kusikiliza, kuchagua na kununua bidhaa mbalimbali kutoka nchi za Afrika.

Utaratibu huu ambao ni mpya, sasa umeanza kuzoeleka kwa wateja mbalimbali wa China.

Shughuli ya mauzo ya bidhaa za Afrika kwa njia ya mtandao wa internet kwa mwaka huu imefanyika rasmi kuanzia tarehe 28 Aprili 28 hadi 12 Mei.

Zaidi ya majukwaa 300 ya biashara ya mtandaoni, yalionesha bidhaa zaidi ya 100,000 kutoka kwa wafanyabiashara zaidi ya milioniĀ  moja wa Afrika na China, katika shughuli hiyo ambayo ni ya nne kufanyika.

Shughuli hii ambayo ni ya nne kufanyika, inataokana na uamuzi wa China kuamua kushughulikia tatizo la urari mbaya wa biashara kati ya China na Afrika.

Also Read
Visa 976 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Licha ya kuwa biashara kati ya pande mbili imekuwa ikiongeza mwaka hadi mwaka, hadi sasa bado upande wa China ndio unauza zaidi bidhaa kwa nchini Afrika kuliko nchi za Afrika, hasa kutokana na kuwa bidhaa nyingi zinazohitajika kwa sasa kwa nchi za Afrika ni bidhaa za mtaji kama mashine na mitambo ambazo hazitengenezwi Afrika.

Kutokana na Afrika kuwa na mazingira mazuri ya kuzalisha bidhaa za kilimo za kitropiki, na wateja wengi wa China kuwa na mwaka wa bidhaa hizo, pande mbili zimetumia hali hii kama fursa ya ushirikiano.

Shughuli ya mauzo ya mwaka huu imeandaliwa kwa pamoja wizara ya biashara ya China, wizara ya Mambo ya Nje, Kamati ya taifa ya Maendeleo na Mageuzi, na Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Habari.

Also Read
Nchi zinazoendelea zinafurahi kuona China na Marekani zinaimarisha ushirikiano wao

Safari hii bidhaa hizi zimetangazwa zaidi katika mikoa ya Hunan, Hubei, Henan na Zhejiang, bidhaa zilizotangazwa zaidi ni zile zinazotoka kwenye nchi 23 za Afrika, ikiwa ni pamoja na kahawa ya Ethiopia, pilipili ya Rwanda na chai ya Kenya, na ufuta kutoka Tanzania.

Kutokana na changamoto ya janga la COVID-19, shughuli za biashara zinazofanywa kwa watu kusafiri kutoka Afrika kuja China zimepungua, lakini maendeleo ya sekta ya habari na mawasiliano yameisaidia kupunguza changamoto hiyo kwa kuwezesha biashara hii kufanyika kwa njia ya mtandao wa internet.

Awamu tatu zilizopita za maonyesho haya zilishirikisha watangaza bidhaa wachina wenye uzoefu, huku baadhi ya maofisa wa balozi na mabalozi wakishiriki kwenye kazi hiyo.

Safari hii baadhi ya watangazaji wa bidhaa hizo ni vijana kutoka nchi za Afrika ambao wana uelewa wa kina kuhusu bidhaa wanazotangaza lakini pia wanaongea kichina fasaha na kuwafahamisha wateja kwa njia rahisi.

Also Read
Joash Onyango Akubali Mkataba Mpya na Simba SC

Hata hivyo licha ya fursa hiyo inayotolewa na serikali ya China na soko kubwa la bidhaa za kilimo za Afrika nchini China, bado soko la China halijatumiwa vizuri.

Changamoto za usindikaji, ufungaji na usafirishaji wa bidhaa hizo bado vinakwamisha bidhaa nyingi za kilimo kutoka Afrika kufika kwenye soko la China. Urahisi wa kukidhi vigezo vya karantini vya China unategemea uwezo wa usindikaji, ufungaji na usafirishaji.

Soko la China ni kubwa na bado linaendelea kuhitaji bidhaa za kilimo kutoka Afrika.

Kama serikali, jumuiya za wafanyabiashara watafanya juhudi kuhakikisha bidhaa mbalimbali za kilimo za Afrika zinaweza kukidhi vigezo vya karantini, bila shaka fursa ya mauzo ya bidhaa za kilimo za Afrika kwenye mtandao wa internet itanufaisha wakulima na wafanyabiashara wengi wa Afrika.

  

Latest posts

Mataifa ya G7 kusitisha uagizaji dhahabu kutoka Urusi

Tom Mathinji

Mzozo wa Ukraine na Russia kujadiliwa katika mkutano wa G7

Tom Mathinji

Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia augua Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi