Billnass asuta waandishi wa habari

Mwanamuziki wa Tanzania William Nicholaus Lyimo maarufu kama Billnass amezomea waandishi wa habari kwa kile alichokitaja kuwa habari za uwongo.

Billnass alikuwa ameandika maneno fulani ambayo yalisababisha mashabiki na waandishi wa habari kukisia kuhusu sababu ya kuachana na Nandy.

Aliandika, “Jamani naombeni sana wanaume tutafuteni pesa kwanza. Hawa wanawake Wana nyodo sana kama wakikuzidi pesa. Mimi yamenikuta nimeamua kujiweka pembeni kwa sasa, I am single now.”

Also Read
Wahu na Nameless washerehekea miaka 23 tangu kuanza kuchumbiana

Alitaja kampuni ya uanahabari ya Global Publishers ambayo iliandika taarifa ikisema kwamba hatimaye Billnass amefichua kilichosababisha yeye na Nandy waachane.

Katika kuwasuta Billnass alisema hajawahi kutangaza hadharani kuhusu hali ya uhusiano wake wa kimapenzi na ni kosa kwa yeyote kukisia na kuandika. Alishauri wanahabari kwenda kupiga hata picha kwenye harusi za watu ikiwa watakosa habari za kuandika.

Also Read
Lil Nas X atetewa na babake kuhusu kutelekeza mamake

Kufikia Sasa Billnass amefuta maneno hayo ambayo aliandika ya kusuta wanahabari.

Mwanamuziki huyo alikuwa amemchumbia mwanamuziki mwenza Nandy ambaye anafahamika kama the African Princess lakini tena Nandy akajitokeza na kusema yuko peke yake.

Also Read
Ushauri wa Professor Jay

Kila wanapoulizwa na wanahabari kuhusu uhusiano wao wa kimapenzi wawili hao hudinda kusema lolote.

Imekuwa muda tangu wawili hao waonekane pamoja hadharani. Waliwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi awali kisha wakaachana baada ya marehemu Ruge Mutahaba kumchumbia Nandy.

Baada ya kifo cha Ruge wawili hao tena wakarudiana.

  

Latest posts

Zuchu Amtania Mamake Khadija Kopa

Marion Bosire

Muigizaji Jaymo Afunga Ndoa

Marion Bosire

Don Jazzy Anatafuta Kumsajili Salle

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi