Bingwa wa olimpiki 2008 Wilfred Bungei azungumzia alivyoshinda uraibu wa pombe

Bingwa wa Olimpiki katika mbio za mita 800 mwaka 2008 mjini Beijing China Wilfred Bungei ndiye mwanariadha wa kwanza aliyejitokeza kimasomaso na kutangaza jinsi alivyotatizwa na alivyokabiliana na uraibu wa pombe .

Kwenye mahojiano ya kipekee na KBC Bungei ambaye kwa sasa anafanya biashara ,anasema kitu kinachowatatiza wanaspoti wengi nchini dhidi ya uraibu wa pombe na mihadarati pamoja  na ulaji muku  ni kutokubaliana kuwa wanalo tatizo.

Also Read
Obiri na Kandie wanyakua ubingwa wa mbio za nyika za KDF

Kilichochangia Bungei kuingilia unywaji pombe kupindukia ilikuwa ni kukosa cha kufanya baada ya kustaafu kutoka riadha.

Also Read
Chepkemoi na Chebolei watwaa ubingwa wa kilomita 10, mbio za nyika mwaka 2022

Mwanariadha huyo ambaye anatoka kwenye familia ya wanariadha waliochochea taaluma  yake ,anasema kuwa alitatizwa na uraibu wa pombe kwa mwaka mmoja unusu  lakini ilimletea madhara mengi kwa familia na pia marafiki huku akikashifiwa kwa kujitokeza hadharani kwa kukiri kuwa na uraibu wa mvinyo.

Also Read
Rwanda Uganda waumiza nyasi bila lengo

Bungei anajivunia kwamba tangu mwaka 2012 hajaonja mvinyo wa aina yoyote  na afya ni bora.

  

Latest posts

Barkane na Pirates kukabana koo Ijumaa fainali ya kombe la shirikisho

Dismas Otuke

Kimeli na Cheptai waibuka mabingwa wa mbio za kilomita 10 za Bengaluru

Dismas Otuke

Timu ya KPA Yakosa Kuingia Fainali

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi