Blue Ivy ashinda tuzo la Grammy huku mamake akiandikisha rekodi mpya

Blue Ivy ni mtoto wa kike wa wanamuziki Beyonce na Jay Z na ameshinda tuzo hilo akiwa na umri wa miaka 9 pekee. Wimbo ambao umesababisha atajwe kwenye tuzo hizo ni “Brown Skin Girl” ambao Blue ameimba kidogo tu na kuonekana kwenye video.

Wanamuziki wengine ambao wamehusishwa kwenye wimbo huo ni Beyoncé, Saint Jhn na Wizkid kutoka Nigeria. Mamake Blue Ivy, Beyonce naye aliandikisha historia mpya kwenye awamu hiyo ya 63 ya tuzo za Grammy ambazo ziliandaliwa mapema leo kulingana na saa za Afrika Mashariki na usiku wa Jumapili tarehe 14 mwezi Machi mwaka 2021 kulingana na saa za Marekani.

Also Read
Mwanamuziki Sosuun aachana na mume wake Kenrazy

Kufikia sasa, Beyonce ameshinda tuzo 28 za Grammy na amekuwa msanii wa kwanza wa kike kuwahi kushinda tuzo nyingi kabisa za Grammy.

Also Read
Wizkid achaguliwa balozi wa mavazi ya michezo ya PUMA

Zamu hii, Beyonce ameshinda tuzo kama vile “Best RnB Performance” kupitia kwa wimbo wake “Black Parade”, “Best Rap Song” kupitia kwa wimbo “Savage” ambao alishirikishwa na Meghan Thee Stallion ambao pia uliwashindia tuzo la “Best Rap Performance”.

Also Read
"Njoro" apata kazi ya Redio
Beyonce na Megan wakipokea tuzo lao

Meghan Thee Stallion, Beyonce na Blue Ivy ni kati ya washindi wachache ambao walikuwepo kwenye ukumbi wa Los Angeles Convention Center mkabala na eneo la kawaida la kuandaa tuzo hizo ambalo ni ukumbi wa Staples na ziliendeshwa na mchekeshaji ambaye pia ni mtangazaji wa runinga Trevor Noah.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi