Bodi ya halmashauri ya KEMSA yafanyiwa mabadiliko

Bodi lote la halmashauri ya usambazaji vifaa vya kimatibabu nchini (KEMSA), limefanyiwa mabadiliko.

Kwenye ilani katika gazeti rasmi la serikali, Rais Uhuru Kenyatta amebatilisha uteuzi wa Kembi Gitura kuwa mwenyekiti wa bodi hiyo na badala yake kumteua Mary Chao Mwadime kuchukua mahala pake.

Also Read
Shughuli ya kurejesha vifaa vya upangaji uzazi aina ya Implanon yakamilika

Mnamo mwezi Machi mwaka huu wa 2020, aliteuliwa kuwa mwenyekiti mpya wa bodi ya  halmashauri ya mawasiliano hapa nchini.

Kipindi cha kuhudumu cha Mwadime kitaanza tarehe 30 mwezi huu kwa muda wa miaka mitatu.

Also Read
Rais Kenyatta na Mama Taifa Margaret Kenyatta wachanjwa dhidi ya Covid-19

Kwenye ilani hiyo hiyo, waziri wa afya Mutahi Kagwe amewateua wanachama wapya wa bodi ya Kemsa watakaohudumu kwa muda wa miaka mitatu kuanzia tarehe 30 mwezi huu.

Hawa ni Lawrence Wahome, Robert Nyarango, Terry Kiunge Ramadhani, na Linkon Nyaga Kinyua.

Also Read
Serikali yajizatiti kukabiliana na visa vya moto Gikomba

Hivyo basi uteuzi wa Timothy Mwololo, Bibiana Njue, Joel Onsare, na Dorothy Atieno kwenye bodi ya KEMSA umebatilishwa.

Hatua hiyo imefuatia sakata ya ununuzi wa bidhaa na huduma katika halmashauri hiyo ambayo inachunguzwa.

  

Latest posts

Nabulindo ashinda kesi ya kupinga kuchaguliwa kuwa mbunge wa Matungu

Dismas Otuke

Kenya yanakili visa vilivyopungua zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Ibada ya wafu ya daktari Gakara na wanawe wawili yaandaliwa Nakuru

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi