Bomba la usambazaji maji katika barabara ya Mombasa kufungwa kwa siku mbili

Kampuni ya usambazaji maji na uondoaji maji taka ya Nairobi, itafunga bomba la usambazaji maji katika barabara ya Mombasa kwa siku 2, kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara ya Express way.

Bomba hilo litafungwa kuanzia kesho saa kumi na mbili asubuhi hadi tarehe mosi mwezi oktoba saa kumi na mbili asubuhi. Kwenye ilani, mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Nahason Muguna, alisema hatua ya kufungwa kwa bomba hilo ni kutoa nafasi kuunganishwa na bomba lingine katika sehemu mbadala yalikohamishiwa mabomba hayo.

Also Read
Jumla ya watu milioni 6,939,559 wamechanjwa dhidi ya COVID-19 hapa nchini
Also Read
Mshukiwa wa utapeli kupitia mtandao wa Amazon Web akamatwa

Alisema sehemu zitakazoathirika na ukosefu wa maji ni pamoja na  JKIA, SGR, Athi River Export Processing Zone, Coca Cola, Mukuru na Imara Daima. Pia mitaa na viwanda katika barabara ya North Airport road, Embakasi village, Tassia estate, General services Unit, kituo cha mafunzo kwa maafisa wa polisi wa utawala na kituo cha mizigo cha  Nairobi inland container depot.

Also Read
Mkataba kati ya benki ya Stanbic na Serikali ya kaunti ya Meru kuwanufaisha wanabiashara

Mitaa mingine itakayoathirika katika barabara ya jogoo ni pamoja na Makadara, Bahati na Maringo na sehemu ya Industrial area.

  

Latest posts

Kliniki mpya ya ugonjwa wa saratani yafunguliwa katika kaunti ya Nandi

Tom Mathinji

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi