Brimin Kipkorir na Agnes Barsosio watwaa ubingwa wa makaka ya kwanza ya Nairobi Marathon

Brimin Kipkorir Misoi na Agnws Barsosio ndio washindi wa makala ya kwanza ya mbio za marathon zilizoandaliwa mapema Jumapili jijini Nairobi.

Kipkorir alikata utepe lwa saa 2 dakika 8 na sekunde 30 akifuatwa na Richard Rop kwa muda wa saa 2 dakika 9 na sekunde 17 huku Daniel Yator akiambulia nafasi ya tatu kwa saa 2 dakika 10 na sekunde 45.

Barsosio aliye na umri wa miaka 39 ameibuka bingwa katika mbio za wanawake akiziparasa kwa saa 2 dakika 29 na sekunde 4 , akifuatwa na Shyline Jepkorir Toroitich kwa saa 2 dakika 29 na sekunde 4 naye Sharon Jemutai akaridhia nafasi ya tatu kwa muda wa saa 2 dakika 29 na sekunde 37.

Also Read
Kenya mbioni kuandaa mashindano ya dunia ya riadha mwaka 2025

Washindi wa marathon walituzwa shilingi milioni 6 nukta 9 kila mmoja huku waliomaliza nafasi za pili wakienda nyumbani na shilingi milioni 4 nao walinyakua nafasi za tatu wakituzwa shilingi milioni 1 nukta 7.

Also Read
Mshikilizi wa zamani wa rekodi ya dunia ya marathon Paula Radcliff atua Kenya

Wanariadha wameshindana kwenye barabara mpya ya Express way ambayo itafunguliwa rasmi kwa matumizi ya uma Jumamosi ijayo.

Bingwa wa Madrid Half Marathon Vincent Ng’etich na Irene Kamais walishinda mbio za nusu marathon .

Mbio hizo zilizoanshishwa rasmi na Rais Uhuru Kenyatta zilikuwa na zawadi ya pesa ya shilingi milioni 45.

Also Read
Kpl yapoteza kesi dhidi ya Fkf

Akihutubu punde baada ya kumalizika kwa shindano la marathon, Rais Kenyatta alielezea matumaini yake kuwa Kenya itafanikiwa kupewa maandalizi ya mashindano ya riadha duniani mwaka 2025.

Kwa upande wake waziri wa michezo Dkt Amina Mohammed ametoa hakikisho kuwa mbio hizo zitaandaliwa kwa kipindi cha miaka 10 ijayo.

  

Latest posts

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Wabunge wa kaunti ya Kitui wataka baa la njaa kutangazwa janga la kitaifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi