Jumanne tarehe 18 mwezi Januari mwaka 2022 itakuwa siku ya wapenzi Brown Mauzo na Vera Sidika kuhalalisha ndoa yao.
Mwanamuziki huyo kutoka pwani ya Kenya Brown Mauzo alitangaza haya kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Alipachika picha ya Vera akiwa amevaa buibui na kujitanda na kuandika maneno “Naoa, Nikah, 18-01-2022, harusi wiki ijayo”.
Vera hajasema lolote kuhusu tangazo hilo lakini wawili hao wamekuwa wakiishi pamoja na Wana mtoto mmoja wa kike kwa jina Asia Brown ambaye ana umri wa miezi mitatu.
Awali Vera Sidika alikuwa amejirejelea kama mke halali wa Brown Mauzo ila hakuthibitisha ikiwa walifanya harusi.
Brown Mauzo naye alikuwa na mke na mtoto kabla ya Kuingia kwenye mahusiano na Vera Sidika.