Bryson Aibuka Mshindi Wa Bongo Star Search

Awamu ya 12 ya shindano la uimbaji la Bongo Star Search ilifika kikomo Ijumaa tarehe 15 mwezi Januari mwaka huu wa 2022 na Bryson Yohana ndiye aliibuka mshindi. Nafasi ya pili ilitwaliwa na Andrew Charles na binti kwa jina Suleiya Abdi ndiye wa tatu. Onyesho la kutangaza washindi lilipeperushwa moja kwa moja kwenye runinga ya Clouds ya Tanzania.

Andrew Charles
Suleiya Abdi

Mgeni wa heshima ambaye alijukumiwa kutangaza washindi kwenye hafla hiyo ni waziri wa maswala ya Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini Tanzania Bwana Mohamed Mchengerwa. Mmiliki wa kampuni ya Benchmark 360 ambayo huandaa Shindano hilo Madam Rita Paulsen ambaye pia ni jaji mkuu wa shindano naye alikuwepo jukwaani wakati wa kutangaza washindi.

Also Read
Mashemeji wamekasirika!

Bi Salama Jabir aliyekuwa mmoja wa majaji alishangaza wengi na muonekano wake kwenye hafla ya jana ambapo alikuwa amevalia sketi. Mara nyingi yeye huvalia suruali.

Also Read
Magawa Atungiwa Wimbo
Bi. Salama Jabir

Awamu ya 12 ya Bongo Star Search ilizinduliwa rasmi Jumatano tarehe 8 mwezi Septemba mwaka 2021 usiku tukio ambalo pia lilipeperushwa moja kwa moja kwenye runinga ya Clouds.

Bi. Jokate Mwegelo mkuu wa wilaya ya Temeke ndiye alikuwa mgeni rasmi na wengine ambao walihudhuria ni Bi. Rita Paulsen, Lil Ommy mtangazaji wa Wasafi Fm aliyekuwa mwongoza mada, mwanamuziki Ommy Dimpoz ambaye alikuwa mmoja wa majaji, mwanamuziki Peter Msechu, washindi wa awamu za awali za shindano hilo kati ya wengine wengi.

Also Read
Ushirikiano wa Koffi Olomide na Diamond Platnumz
Madam Rita

Baada ya uzinduzi, shughuli ya kutafuta washindani ikaanza rasmi tarehe 25 mwezi Septemba na kukamilika tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka 2021. Majaji walizuru maeneo ya Arusha, Mwanza, Mbeya, Dodoma, Zanzibar na Dar es Salaam kutafuta washindani.

  

Latest posts

Brown Mauzo Azindua Video ya Kibao “Naoa”

Marion Bosire

Wadau wa Filamu Wahimizwa Kutoa Mawasilisho ya Warsha ya Durban

Marion Bosire

Akothee Atangaza Ziara

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi