Bunge la Kaunti ya Uasin Gishu lafungwa kwa muda kutokana na hofu ya COVID-19

Spika wa Bunge la Kaunti ya Uasin Gishu David Kiplagat amesimamisha vikao vya bunge hilo kwa siku 21.

Hii ni baada ya kubainika kwamba aliyekuwa Mwakilishi wa Wadi ya  Huruma Peter Kiiru Chomba alifariki kutokana na ugonjwa wa COVID-19.

Akiongea kwenye afisi za bunge hilo kwenye hafla ya mpango wa mazishi ya marehemu, Kiplagat amewashauri wawakilishi wa wadi kujitenga wakati wa kipindi hicho.

“Wakati wa kipindi hicho, wawakilishi wadi na wafanyikazi wengine watajitenga. Tuanasihi kila mmoja aendelee kuzingatia kanuni za Wizara ya Afya,” akasema Spika huyo.

Also Read
Mswada wa BBI kuwasilishwa katika Bunge la Kitaifa Alhamisi
Also Read
Bunge kurejelea vikao baada ya likizo ya wiki mbili

Gavana wa Uasin Gishu Jackson Mandago, ambaye amehudhuria mkutano huo, ametoa wito kwa wakazi kuzingatia masharti yaliotolewa na Wizara ya Afya ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa korona.

Mandago amesema hali ya sasa ambapo watu wanapuuza masharti hayo imepelekea kuongezeka kwa visa vya maambukizi.

Also Read
Serikali za kaunti zahimizwa kuongeza vitengo vya kuwahudumia wagonjwa mahututi

“Kumekuwa na ulegevu katika kuzingatia masharti ya COVID-19. Nimetembea mjini, watu hawazingatii tena kukaa mbali mbali, kunawa mikono au kuvaa barakoa,” amesema Mandago.

Ametoa wito kwa wanasiasa kuwa mfano bora kwa kuzingatia masharti hayo ili kusaidia kupunguza visa vya maambukizi ya ugonjwa huo.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi