Bunge la Kitafa na lile la Senate zatakiwa kusuluhisha tofauti baina yazo

Rais Uhuru Kenyatta amehimiza  bunge la kitaifa na lile la Senate kushirikiana katika kusuluhisha changamoto baina yazo.

Akizungumza katika majengo ya bunge wakati wa hotuba kwa taifa ya mwaka 2020, Rais alisema mtafaruku hushuhudiwa katika mabunge mawili huku kila moja likijizatiti kutekeleza majukumu yake ya kikatiba.

Also Read
Wabunge wa kike na wa kiume watofautiana kuhusu ushauri wa Maraga wa kuvunja bunge

Kwa mujibu wa Rais, uongozi wa taifa hili uko tayari kuleta uwiano na kutafuta suluhu zinazoathiri mabunge hayo.

Himizo hilo la Rais linajiri huku mabunge yote mawili yakionyesha ubabe wao baada ya mahakama kufutilia mbali sheria 23 zilizopitishwa na bunge la kitafa bila kuhusisha bunge la Senate.

Also Read
Peter Kenneth: Mlima Kenya uko huru kuwa na mgombeaji Urais

Bunge la Senate lilipinga mahakamani hatua ya bunge la kitaifa kupitisha sheria hizo.

Jopo la majaji watatu lilifutilia mbali upitishaji sheria hizo 23 hadi pale bunge la Senate litakapohusishwa.

Also Read
Ziara ya Rais Kenyatta nchini Uingereza kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili

Hata hivyo bunge la taifa lilisema litakata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, likidokeza huenda ikasababisha changamoto za kikatiba kwa kuwa baadhi ya sheria hizo tayari zinatekelezwa.

  

Latest posts

Wakazi wa Nandi ya kati wahimizwa kushirikiana na polisi kukabiliana na uhalifu

Tom Mathinji

Serikali yahimizwa kutoa mikopo ya HELB kwa wanafunzi wa vyuo vya kibinafsi

Tom Mathinji

Mahakama iko tayari kwa kesi za uchaguzi mkuu ujao asema Jaji mkuu Martha Koome

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi