Bunge la Kitaifa laidhinisha uteuzi wa Martha Koome kuwa Jaji Mkuu

Bunge la kitaifa limeidhinisha kwa kauli moja uteuzi wa Martha Koome kuwa Jaji Mkuu humu nchini.

Koome alisailiwa na kamati ya masuala ya haki na sheria katika bunge la kitaifa inayoongozwa na Muturi Kigano juma lililopita.

Also Read
Mbunge Oscar Sudi kuzuiliwa korokoroni siku mbili zaidi

Mapema leo, kamati hiyo iliwasilisha ripoti yake bungeni kwamba ilikubali uteuzi wa Koome kuchukua wadhifa huo.

Wabunge wamejadili ripoti hiyo na hatimaye kupiga kura na kuidhinisha uteuzi wa Koome kuwa Jaji Mkuu.

Also Read
Poghisio awalaumu wanasiasa kwa kuchangia kuenea kwa virusi vya korona

Spika wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi anatarajiwa kuwasilisha rasmi ripoti ya kuidhinishwa kwa Koome kwa Rais Uhuru Kenyatta, ambaye atachapisha uteuzi rasmi kwa gazeti rasmi la serikali.

Also Read
Maraga asifu mfumo wa dijitali wa shughuli za mahakama

Atakapoapishwa, Jaji Koome atakuwa Jaji Mkuu wa 15 humu nchini na wa kwanza mwanamke, hivyo kuchukua nafasi iliyoachwa na David Maraga aliyestaafu kutoka wadhifa huo mnamo Januari mwaka huu.

 

  

Latest posts

ODM yashutumu vikali ghasia za Migori dhidi ya Jimi Wanjigi

Tom Mathinji

Prof. Magoha: Mtaala mpya wa elimu hautatupiliwa mbali

Tom Mathinji

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi