Bunge la Seneti lapitisha mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020

Bunge la seneti limepitisha mswaada wa marekebisho ya katiba mwaka 2020 maarufu kama BBI.

Maseneta 51 wamepiga kura ya kuidhinisha mswaada huo, ilhali 12 walipinga huku mmoja akikosa kupigia upande wowote kura.

Waliounga mkono mswaada huo walisema mabadiliko yaliyopendekezwa yatawafaidi wakenya ila walioupinga walihoji kuwa mswaada huo – ikiwa utapitishwa kuwa sheria jinsi ulivyo – utakuwa mzigo kwa wakenya kufuatia nyadhifa zaidi za uongozi zilizopendekezwa.

Also Read
Raila awashtumu wanaokosoa mpango wa BBI

Huku akiwapa kongole maseneta kwa kuuptisha mswaada huo seneta wa siaya James Orengo, alisema semi zao kuhusu wema wa mswaada huo zitarejelewa katika siku za usoni.

Seneta wa Nairobi Johnson Sakaja na mwenzake wa Bungoma Moses Wetangula walitoa wito kwa maseneta wenzao licha ya miegemeo yao kisiasa kuwaunganisha wakenya na kuwahamasisha zaidi kuhusu mswaada huo maarufu kama BBI.

Also Read
Wanaopinga BBI watahadharishwa dhidi ya kueneza propaganda

Kura hiyo ya kuupitisha mswaada huo katika seneti imejiri siku chache baada ya ile iliyopigwa katika bunge la kitaifa siku ya Alhamisi ambapo mswaada huo ulipitishwa na wabunge wengi.

Also Read
Halfa ya uzinduzi wa ripoti ya BBI yang’oa nanga Bomas

Kabla ya kuutia Saini mswaada huo kuwa sheria, Rais atauwasilisha kwa tume ya uchaguzi IEBC ambayo itaanda kura ya maoni ndani ya siku 90.

Wakati huo huo, kiongozi wa upinzani Raila Odinga amewapongeza wabunge na maseneta kwa kupiga kura ya kuunga mkono mswaada wa BBI kwa wingi.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi