Bunge la Seneti lapokea azimio la Kumtimua Sonko mamlakani

Wakaazi wa Nairobi huenda wakalazimika kurudi uchaguzini ili kumchagua gavana mpya ikiwa bunge la Seneti litaidhinisha hoja ya kumwondoa afisini gavana Mike Sonko.

Hii ni baada ya bunge la Seneti Ijumaa kupokea azimio la bunge la kaunti ya Nairobi la kumfurusha gavana huyo anayekumbwa na utata.

Azimio hilo lilimtuhumu Sonko kwa matumizi mabaya ya mamlaka,  utovu wa maadili na ukiukaji wa katiba.

Also Read
Hatma ya Sonko kuamuliwa kwenye kikao cha pamoja cha Seneti

Hoja hiyo ilipitishwa kwenye kikao cha Alhamisi alasiri na wanachama 88 wa bunge la kaunti ya Nairobi.

Ni wanachama wawili pekee waliopinga hoja hiyo iliyowasilishwa na kiongozi wa walio wachache kwenye bunge hilo, Michael Ogada.

Sonko alitarajiwa kujitetea bungeni kabla ya kura hiyo kupitia mtandao lakini hakufanya hivyo.

Also Read
Wakili wa Sonko kwenye kesi ya ufisadi ajiondoa

Badala yake gavana huyo alikuwa katika kaunti ya Kwale akiandamana na baadhi ya wanachama wa bunge hilo waliopinga hoja ya kumbandua afisini.

Sonko alikataa kuidhinisha bajeti ya kaunti ya Nairobi akisema haifai kwa wanachama wa bunhe hilo kutenga kitita cha shilingi bilioni-27 kati ya shilingi bilioni-37.5 kwa halmashauri ya usimamizi wa jiji la Nairobi.

Also Read
Siogopi kung'atuliwa mamlakani,Mike Sonko afoka

Ogada alisema kuwa bunge hilo halikuwa na budi ila kumtimua gavana Sonko.

Hatua hii ya kumbandua gavana sonko imejiri miezi michache baada ya jaribio sawia na hilo ambapo Sonko alienda mahakamani mwezi Machi na kusimamisha njama hiyo ya baadhi ya wabunge wa bunge la Nairobi.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi