Bunge ladinda kumwondoa Tabitha Mutemi kutoka bodi ya baraza la vyombo vya habari nchini

Wabunge katika bunge la taifa wametupilia mbali ripoti ya kamati ya habari,mawasiliano na ubunifu inayopendekeza kuondolewa kwa Tabitha Mutemi kutoka bodi ya baraza la vyombo vya habari nchini.

Wakikataa ripoti ya kamati hiyo inayoongozwa na William Kisang,wabunge Sabina Chege,Otiende Amollo na Godfrey Osotsi, walisema hawakuridhika na mchakato mzima wa utayarishaji ripoti hiyo.

Also Read
Viongozi wa Murang'a kuhudhuria mikutano yote ya kisiasa katika kaunti hiyo

Hayo yalijiri huku kukiwa na madai kwamba Mutemi hakupewa nafasi ya kujieleza.

Wabunge walisema kama mwanabodi wa baraza la vyombo vya habari,Mutemi hahusiki moja kwa moja katika shughuli za baraza hilo,na hivyo basi hakuna ukiukaji wowote wa maadili ya utumishi wa umma.

Also Read
Akina mama na watoto wenye akili taahira wapokea msaada wa vyakula na mavazi kutoka Women Empowerment Kenya

Walisema bunge halifai kutumiwa kusuluhisha tofauti za binafsi.

Wakati spika wa bunge la taifa Justin Muturi alipowasilisha pendekezo hilo,wabunge walipinga.

Also Read
Serikali yabuni kamati yakushughulikia Usalama na Utangamano wa umma

Bunge lilikuwa limehimizwa kusaidia kutanzua mzozo kuhusu uanachama wa Mutemi katika bodi ya baraza la vyombo vya habari,ilhali yeye ni mfanyakazi wa tume ya uchaguzi nchini,IEBC.

  

Latest posts

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi