Bunge latakiwa kupitisha mswada kuhusu mihadarati kabla ya msimu wa sherehe

Aliyekuwa mwenyekiti wa shirila la NACADA, John Mututho amelitaka bunge kupitisha mswada wa kukabiliana na mihadarati kabla ya kwenda mapumzikoni.

Mututho amesema visa vya ghasia katika Kaunti za Nakuru na Kiambu vimetokana na matumizi ya mihadarati miongoni mwa vijana waliosalia nyumbani kutokana na chamko la Korona.

Also Read
Serikali kushirikiana na Kanisa katika utoaji huduma kwa Wakenya

Aidha, Mututho amesifia bunge la 12 kwa kufanyia marekebisho sheria za jadi kuhusu mihadarati zilizolegeza  adhabu dhidi ya walanguzi na wasambaji wa mihadarati.

Akiongea na wanahabari mjini Naivasha, Mututho alisema inawezekana kupitisha mswada huo kuwa sheria kabla ya msimu wa sherehe kuanza.

Also Read
Jiko la makaa lasababisha vifo vya jamaa watano Ruiru

“mswada huo utasomwa kwa mara ya pili Jumanne na wabunge wanaweza kuupitisha utakaposomwa mara ya tatu ukisubiri kuidhibnishwa na rais,” alisema Mututho.

Mututho alidokeza kuwa mswada huo unapendekeza adhabu kali kwa wauzaji mihadarati akisema hatua hiyo itasuluhisha tatizo lililopo la utumizi wa dawa za kulevya hapa nchini

Also Read
Shughuli zaidi za sehemu ya kwanza ya Bandari ya Lamu kuanza mwezi Juni

Mbunge wa Nyali Mohammed Ali ndiye aliyewasilisha katika bunge la kitaifa mswada wa marekebisho ya sheria ya mwaka 2019, kuhusu mihadarati.

 

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi