Burna Boy arejea nyumbani baada ya ushindi wa Grammy

Mwanamuziki huyo wa taifa la Nigeria alirejea nyumbani katika jimbo la River, juzi baada ya ushindi wake kwenye tuzo za kimataifa za Grammy.

Alipokelewa kwa njia ya kipekee na mashabiki wake katika jimbo alikozaliwa la River na hata usimamizi wa jimbo hilo ukiongozwa na Gavana Nyesom Wike.

Video kadhaa zilichapishwa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha mashabiki wakishangilia msafara wa mwanamuziki huyo na nyingine zikionyesha akiwa na Gavana na viongozi wengine nje ya afisi kuu za jimbo.

Also Read
Wizkid ashinda tuzo la msanii bora wa mwaka

Mamake kwa jina Bose Ogulu ambaye ni meneja wake alikuwa ameandamana naye.

Akizungumza huko Port Harcourt, River State, Burna Boy, ambaye jina lake halisi ni Damini Ogulu alisema kwamba ukaribisho aliopata na mapenzi aliyoonyeshwa na watu wa nyumbani pamoja na serikali ya jimbo unazidi tuzo lolote.

Also Read
Babake Nicki Minaj auawa kwenye ajali

Gavana Nyesom Wike alimtaja Burna Boy kuwa fahari ya jimbo la River na akatoa ahadi ya kumpa usaidizi wa kuendeleza kazi yake ya muziki.

Also Read
Hafla ya ukumbusho wa DMX kuonyeshwa mtandaoni

Burna Boy alishukuru Gavana kwa kutumia muda wake kumwandalia makaribisho ya aina yake huku Gavana akisema kila mmoja jimboni humo anajivunia ufanisi wa Burna Boy.

Burna Boy alishinda tuzo la Grammy katika kitengo cha albamu bora ya ulimwengu kwenye awamu ya 63 ya tuzo hizo za kimataifa.

  

Latest posts

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Eduswagga Azungumzia Safari Yake Ya Muziki

Marion Bosire

Tory Lanez Afuta Instagram Kulikoni?

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi