Bwawa la amani kuunganisha jamii za Turkana,Pokot na Karamoja

Kukamilika kwa ujenzi wa bwawa la mamilioni ya pesa huko Kasses katika kaunti ndogo ya Pokot Kaskazini kunatarajiwa kumaliza mizozo ya kijamii na kuwapa wafugaji maji safi.

Hii inafuatia mpango wa amani uliotiwa saini kati ya rais Uhuru Kenyatta na rais Yoweri Museveni wa Uganda huko Moroto mnamo 2019.

Also Read
Serikali kujenga jumba la mikutano kwa gharama ya shilingi bilioni 1.4 kaunti ya Kisumu

Mpango huo ulilenga kumaliza mizozo ya mipakani kati ya jamii ya Turkana, Pokot na Karamoja na kukuza maendeleo.

Waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa akiwa katika ziara katika sehemu hiyo, alibaini kuwa mradi huo utakomesha wizi wa ng’ombe.

Also Read
Familia kadhaa zakosa makao kutokana na Mafuriko Migori

Bwawa hilo la amani ni miongoni mwa mengine kadhaa huko Turkana na Marsabit ambayo ni miradi muhimu iliyoanzishwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Also Read
Shujaa yaipakata Canada alama 24-5 katika msururu wa Seville Uhispania na kufufua matumini ya kutinga robo fainali

Katibu wa Ugatuzi na Maeneo Kame, Micah Powo, alisema kuwa bwawa hilo lililojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 250 lina uwezo wa kuhifadhi lita bilioni 1.2 za maji na litahudumia familia alfu tisa.

  

Latest posts

Atlas Lions ya Moroko yaiparuza Ubelgiji Kombe la Dunia

Dismas Otuke

Rais Ruto: Kenya ina uwezo wa kujiendeleza kiuchumi

Tom Mathinji

Visa 36 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi