Cameroon na Mali watinga robo fainali CHAN huku wapinzani wao wakibainika Jumatatu

Wenyeji Cameroon almaarufu Indomitable Lions na Flying Eagles ya Mali zilikuwa timu mbili za kwanza kutinga robo fainali ya makala ya 6 ya michuano ya CHAN Jumapili usiku.

Cameroon walinusirika fedheha kutoka kwa  Burkina Fasso katika mechi ya kundi A iliyosakatwa kiwarani Ahmadou Ahidjo na kutoka sare tasa iliyohakikisha wanamaliza katika nafasi ya pili kwa alama 5 huku Bukinafasso wakiyaaga mashindano kwa kutwaa nafasi ya tatu.

Also Read
Mashindano ya dunia ya mbio za Nyika yaahirishwa hadi mwaka 2022

Kwenye mkwangurano mwingine wa kundi  A uliochezwa sambamba uwanjani Reunification mjini Doula, Mali  walihitaji goli la dakika ya 12 lake Demba Diallo ili kuongoza kwa alama 7 .

Timu mbili kuingia hatua ya nane bora kutoka kundi B zitabainika Jumatatu usiku mabingwa mara mbili DR Congo wakichuana na Niger katika uwanja wa Ahmad Ahidjo mjini Younde , ambapo Wakongo wanahitaji sare kufuzu kwa robo fainali  baada ya kushinda mchuano mmoja na kwenda sare mmoja.

Also Read
FKF yasukuma mbele kuanza kwa ligi kuu kutoka Mei 12 hadi Mei 14

Mechi nyingine ya kundi hilo itakuwa baina ya Red Devils ya Congo Brazaville dhidi ya Mediterranean Knights ya Libya  uwanjani Japoma mjini Doula ikiwa mechi ya tatu kati ya pande hizi mbili ,michuano ya awali ikiishia sare ya 2-2 na 1-1.

Also Read
Brian Mandela ajiunga na Mamelodi Sundowns kwa mkataba wa miaka mitatu

Mechi za makundi zitakamilika Jumatano kabla ya kupisha kwota fainali baina ya Jumamosi na Jumapili hii.

 

 

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi