Cardi B na Megan Thee Stallion kutumbuiza kwenye Grammys

Cardi B, Megan Thee Stallion, Lil Baby, Doja Cat na Brittany Howard ni baadhi tu ya wasanii ambao watatumbuiza kwenye hafla ya 63 ya tuzo za Grammy Jumapili tarehe 14 mwezi Machi mwaka huu.

Mchekeshaji wa asili ya Afrika kusini ambaye pia huendesha kipindi kiitwacho “The daily show” Trevor Noah ndiye ataendesha tuzo hizo za Grammy.

Megan The Stallion, ambaye ameteuliwa kuwania tuzo za mwaka huu za Grammy kwenye vitengo vinne ambavyo ni “Rekodi ya mwaka”, “Msanii bora mpya”, “Onyesho bora la rap” na “wimbo bora wa Rap”, alijulikanisha haya kupitia Twitter.

Also Read
Tuzo za Kalasha

Aliandika, “Nina furaha hatimaye kuwatangazia kwamba nitatumbuiza kwenye hafla ya tuzo za Grammy tarehe 14 mwezi Machi mwaka huu. Jiwekeni tayari.”.

Hafla hiyo itapeperushwa moja kwa moja kutoka ukumbi wa “Staples Center” ulioko Los Angeles nchini Marekani na kuonyeshwa kupitia Paramount +. Tuzo hizo awali zilikuwa zimepangiwa kuandaliwa tarehe 31 mwezi januari mwaka huu lakini zikaahirishwa kutokana na kuongezeka kwa visa vya maambukizi ya virusi vya Corona.

Also Read
Diamond amwombea mema Haji Manara

Waandalizi wa tuzo hizo wakitangaza kuahirishwa kwa hafla hiyo walisema kupitia ujumbe wa pamoja kwamba walichukua hatua hiyo baada ya kushauriana na wataalam wa maswala ya afya, mwendesha sherehe na wasanii ambao walikuwa wamepangiwa kuhudhuria.

Wakati huo huo waandalizi hao wametangaza kwamba hafla ya mwaka huu ya kutuza washindi wa Grammys itatilia maanani kanuni za kuzuia kusambaa kwa Covid 19.

Tofauti na jinsi imekuwa kwenye hafla za awali za kutuza washindi, mwaka huu wafanyi kazi wa hoteli ya Troubadour and Hotel Cafe iliyoko Los Angeles, wale wa ukumbi wa maonyesho wa Apollo mjini New York na wa Nashville Station Inn ndio watapokeza washindi tuzo zao.

Also Read
Idris Sultan atania Nandy na Koffi

Mwanamuziki Beyoncé anaongoza kwa upande wa kina dada kwa kuteuliwa kuwania tuzo kwenye vitengo vingi ambavyo ni tisa na Roddy Ricch anaongoza kwa upande wa wanaume kwa kuteuliwa kuwania tuzo kwenye vitengo tisa pia.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi